Xiaomi ni jina la kampuni na kwa sasa inatengeneza simu katika brand 3 tofauti: Xiaomi(hizi zinabeba jina la kampuni mama), Redmi na Poco. Xiaomi wanatengeneza flagship , Redmi na Poco ni sub brand zao ambazo zimejikita kutengeneza simu nzuri kwa gharama za chini. Zote ni simu nzuri, bajeti yako na preference zako ndio zitaamua ununue Xiaomi, Redmi au Poco ila zote experience ni ileile, tofauti ni kwamba Xiaomi ni more premium, Redmi na Poco ni midrange nzuri, low end pia wanazo
Kama una budget ya chini Redmi na Poco wana simu nzuri sana na zenye very capable hardware kuliko washindani. Kwa hiyo zote ni nzuri cha msingi zinatoa product bora kulingana na bei.
Kwa mfano kama unataka simu ya Xiaomi, unaweza sema budget yako ni kiasi gani?