Februari 20: Siku ya Kimataifa ya Haki za Kijamii (Social Justice Day)

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Haki ya Kijamii Humaanisha uwepo wa Haki sawa kwa watu wote na uwezekano wa kila mtu, bila ubaguzi, kufaidika na Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii Duniani kote

Ni mtazamo kwamba kila Mtu anastahili Haki na Fursa sawa. Baadhi ya Haki za Kijamii ni pamoja na kushiriki Uchaguzi, Usawa wa Fursa za Kiuchumi, Usawa mbele ya Sheria na Haki ya kupata Huduma za Afya

Haki ya Kijamii inakuza Haki na Usawa katika nyanja nyingi za Jamii

Siku ya Kimataifa ya Haki ya Kijamii ni Siku inayoangazia hitaji la kukuza Haki za Kijamii ambazo zinahusisha jitihada za kushughulikia masuala mbalimbali kama Umasikini, Ukosefu wa Usawa wa Kijinsia, Ukosefu wa Ajira na HakiZaBinadamu

Siku hii huadhimishwa kila Februari 20, ikilenga kupaza sauti dhidi ya dhuluma za Kijamii zinazotokea duniani kote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…