Yussufhaji
Member
- Sep 9, 2018
- 35
- 28
13/04/2022
Pablo Escobar, mlanguzi nguli wa madawa ya kulevya mwenye asili ya Colombia alikuwa akitumia maneno hayo mawili kuelezea njia anayoitumia katika kufanikisha biashara haramu za madawa ya kulevya. Neno Plata likiwa na maana ya "Fedha" na Neno Plomo likiwa na maana ya "Risasi". Pablo Escobar alikuwa akiwapa option maafisa wa serikali wachague kati ya kupokea rushwa au kupoteza maisha yao, ilimradi afanikishe biashara zake!
Kwanini "Plata O Plomo"?
Hivi karibuni, Rais Joe Biden wa Marekani alipokuwa ziarani Poland, vyombo vya habari mbalimbali vilimnukuu akitamka:-
"Kwa ajili ya Mungu, (Putin) hawezi kubaki madarakani"
Kauli ambayo Ikulu ya Washington iliikana, japo iliengeza maswali juu ya sera ya mambo ya nje ya Marekani pale kiongozi wa nchi nyengine huru anapokwenda tofauti na maslahi ya Marekani,
Katika hali isiyo ya kawaida, mshirika muhimu na wa muda mrefu wa Marekani barani Asia, India, iliamua kutoegemea upande wowote katika upigaji wa kura azimio dhidi ya operesheni ya kijeshi ya Urusi nchini Ukraine, na baadaye katika baraza la haki za binaadamu nchi hiyo pia iliamua kutoegemea upande wowote pale azimio la kuiondoa Urusi katika Baraza la Haki za binaadamu lilipowasilishwa. Marekani inaonekana dhahiri kabisa kuhadhabishwa na hatua hiyo ya India, huku mshauri wa masuala ya uchumi wa Rais Biden, Brian Deese akinukuliwa:-
"India imearifiwa athari za kujiegemeza na Moscow zitakuwa wazi na za muda mrefu"
Kauli ambayo inachukuliwa kama ni onyo kwa India,
Huko Pakistani, bunge la nchi hiyo lilipiga kura ya kutokuwa na imani na aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Bwana Imran Khan awali vyombo vya habari vya ndani ya Pakistani viliripoti juu ya ujumbe aliopewa aliyekuwa balozi wa Pakistani Washington na mmoja ya viongozi waandamizi wa Washington kuwa Washington inafikiri uhusiano wao utakuwa mzuri iwapo Khan ataondoka ofisini, Imran khan alinukuliwa akieleza kuwa Washington inapanga njama dhidi yake baada ya nchi yake kupiga kura ya kutoegemea upande wowote katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Imran khan alinukuliwa akiuliza "Sisi ni watumwa wenu?" "Mimi tu, nikiondoka, kila kitu kitasamehewa". Washington inakana madai hayo.
Kwa maoni yangu binafsi, ni wazi kuwa, Ikulu ya Washington inafanya kila iliwezalo, kila lililo ndani ya uwezo wake kuhakikisha Moscow inatengwa na jamii ya kimataifa,
Washington imekuwa ikifulululiza mtiririko wa vikwazo kwa Moscow huku ikiitaka jamii ya kimataifa kufuata hatua zake na kuzionya baadhi ya nchi kama China iwapo itaisaidia Urusi kupambana na makali ya vikwazo vya Washington basi itakiona cha mtema kuni huku Washington ikiwashajihisha washirika wake wa Magharibi kwa ahadi kedekede za mafuta na ulinzi,
Ni wazi kabisa, ni Fedha au Risasi!
NB: Maoni yangu binafsi katika sura ya siasa za kimataifa kwa hivi sasa.
Na
@Syn_krest'yanina
Email; Hajjyussuf2@gmail.com
WhatsApp: wa.me/+255777158131