Fedha za field zimekuwa majanga !

Freyzem

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2013
Posts
10,120
Reaction score
24,667
Hii ni wiki ya tatu tokea mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu yaanze, lakini fedha za mafunzo hayo ambayo loan board iliingia mkataba na hao wanafunzi hawajapatiwa! wanafunzi wapo maporini, wengine wapo sehemu ambazo hata ndugu hawana wanateseka kwa njaa! jamani huu siyo ubinadam..

baadhi ya vyuo ambavyo havijapewa hizi fedha ni udsm(conas, coet, cohu, coss), st Augustine, udom na vingine.

Jaman hebu serikali iwaonee huruma hawa vijana wanaosoma ili waijenge nchi kwa kuwapatia fedha zao!!
 
Jamani hivi kumbe tunasoma huku tunategemea serikali 100%?

Ina maana support ya ndugu na jamaa itakuja kuonekana lini..? siku tukiwa na kazi ama?

Btw, wanafunzi nao wana matumizi mabovu sana ya pesa, pesa ya boom ina uwezo wa kutumiwa vizuri kabisa na ku-cover RISKS kama hizi... mpe mwanafunzi sasa uone, mwezi mmoja tu pesa imeisha, kilichofanyika utakuta ni nje kabisa ya pesa ilichopangiwa, achilia mbali wale wanaosaidia ndugu zao kwa hizo pesa, lakini hilo nalo halikuwa lengo...

Hata hizo pesa za field nazo wengi wakipewa huwa zinaisha hata kabla ya muda wa field, kwani uongo?

MATUMIZI YA PESA KWA WANAFUNZI WA VYUO NI MABOVU SANA, TUSEME UKWELI TU, SIO LAWAMA KILA SIKU.....!

we ngoja uone vyuo vikifunguliwa, watu watadai pesa fasta kama vile walikuwa wanalala njaa ama wamefukuzwa kwao, hata wiki haipiti..

JAMANI EENH, MNAPOPEWA PESA, IWE NI YA M.A ama FIELD, JARIBUNI KUTUNZA JAPO KIASI KIDOGO CHA KUWASAIDIA HAPO BAADAE KWA RISK KAMA HIZI,

WENGINE HATA VYUO WAKISHAHITIMU WANAKOSA MPAKA NAULI... STAREHE ZITAWAMALIZA..
 
Jamani hivi kumbe tunasoma huku tunategemea serikali 100%?

Ina maana support ya ndugu na jamaa itakuja kuonekana lini..? siku tukiwa na kazi ama?

Kwa paragraph hii nakushauri tembea hii tanzania ujue maisha ya watu wake. Inaonekana wee umezaliwa, umekulia na unaishi mjini.

Mshukuru Mungu sana kwa bahati hiyo. Ila usiwadharau wenye shida, hawakuumbiwa shida.
 
Mkuu EXCEl: ukipewa laki nne na nusu kwa miezi miwili na ushee utabakisha kias gan?. Udsm( mabibo hostel), nauli to and fro tsh.800, brk fast 1500, lnch 2000, dinner 2000, maji (mchna na jion) 1200, sabuni, vocha atlst 1000 per 2dyz, pango 750 per day, bado hpo crdb wananakato yao.

Kumbka loan bord wanatoa 75000 for meals and accmdtion kwa siku 1 ambyo n sawa na lak 4 na nusu kwa miezi miwili yenye jumla ya siku 60, je n vp kwa miezi miwil yenye cku 61?.

Kimsingi pesa kwa ajili ya meals na accomodation haitsh hta kidogo ss iv gharama za maisha zimepnda tofaut na miaka ya nyuma jamani.
 

Mkuu umetisha! yani chakula cha asubuhi unakula 1500? ni nini hicho we mwanafunzi unakula? unafanya kazi TRA mkuu?

lunch 2000 na dinner 2000? maji mchana na jioni 1200, hapa ongezea na 1500 ya BF jumla 7700!

Mkuu mbona una matumizi mabovu hivi kwa kulisha tumbo lako? kwani lazima ushushie soda na juice kila siku?

Vyakula vingi sidhani kama kuna kinachovuka shs 1500 kwa lunch and dinner kwa wanafunzi.. wewe naona umeamua kuongeza cost hewa tu hapa..

Hizo vocha unazoweka zilipangwa na serikali mkuu? hebu tuwe wawazi, kuna matumizi mengine tunayaweka kiasi kwamba tunajiumiza wenyewe...

Transport cost inategemea na wewe unaishi wapi, hiyo sikatai inaweza fika mpaka 800 ama kuzidi kwa siku..

Lakini tuseme ukweli, shs 7500 kwa ajili ya mlo na malazi hazitoshi kweli?

umepewa shs 2500 ambayo ni sawa na shs 75000 kwa mwezi kwa ajili ya malazi, kuna chumba kinazidi hiyo bei hapa mjini kwa mwanafunzi? kama kuna mazidi, kwanini msichangie muishi wawili?...

shs 5000 kwa ajili ya chakula.. 1000 asubuhi, 1500 mchana na 1500 usiku, baki 1000 ya ziada kwa maji nk,

serikali sidhani kama itapiga mahesabu ya kukupa surplus hata siku moja..

Mkuu, wanafunzi wa vyuo tuna matumizi ya pesa mpaka sehem zisizohusika.. CLUB ni sisi, BEACH kila weekend ni sisi, BASH za hapa na pale ni sisi... kwa hiyo hiyo 7500! lazima tutalia njaa tu!
 
Kwa paragraph hii nakushauri tembea hii tanzania ujue maisha ya watu wake. Inaonekana wee umezaliwa, umekulia na unaishi mjini. Mshukuru Mungu sana kwa bahati hiyo. Ila usiwadharau wenye shida, hawakuumbiwa shida.
asante mkuu kwa ushauri, ila ukweli utabaki kuwa,

wanafunzi wa vyuo, wengi wetu tuna matumizi mabovu sana ya pesa.. nadhani kuna watu hawajawahi kushika pesa nyingi nyingi hivi kwa siku moja, jiulize hii misimu ya gharama tunaitoa wapi wakati mwanzo hatukuwa nayo???

Halafu jiulize tena, hii misimu ya gharama inaenda wapi baada ya kuhitimu masomo?.. inauzwa tupate pesa!

mbona watu wanaweza kusev pesa wanunue laptops na smartphones? kwanini isiwezekane mtu utunze pesa for better future use??

wakati ufike tujifunze... Boom halina mashetani wala nini kama tunavyodai, mashetani tunayo sisi wapokea boom!
 
mkuu Kingmairo,

tusiende mbali sana, najua kuna ndugu zetu wanajisomesha hapa vyuoni kwa kutumia boom hili hili, wala hilo sina shaka nalo,

najua wazi kabisa maisha si tambarare kwa wote, wengi wetu walioko vyuoni wanasomesha wadogo zao huko chini,


lakini ukweli utabaki pale pale, allocation of money kwa wengi wetu bado ni janga, kuna jamaa mmoja nilianza nae chuo mwaka juzi, alipopewa pesa tu, breki ya kwanza ilikuwa mlimani city for shopping..!!!!!!! imagine such a person!

Baada ya shopping akaanza kusambaza love kwa wenzake, kwa pesa ile ile ya boom!.. kimbembe kikaja baada ya pesa kukatika kabla ya muda... najua unajua kitakachofuata...
 
Last edited by a moderator:
polen sana duuu nishaga sahau hekaheka za chuo. ati kufundisha ni wito pia inaelezwa kama ni kazi ya mungu hivyo hamna budi kuifanya kwa moyo poleni sana
 
Mimi sio mwanachuo lakini ninamuunga mkono msemaji hapo juu kuwa wanachuo wanapopata boom hutumia kwa pupa kana kwamba wanakufa punde.

Lakini pia kutumia pesa hovyo sio sababu ya kumcheleweshea mwanachuo pesa yake. Wapewe mambo ya matumizi ni suala binafsi. Hayatuhusu ki hivyo.
 
Mkuu unavyoandika ufikirie kidogo, kumbuka hiyo pesa sio kila mtu anaitumia kwa anasa kama unavyodhani. Umesema ndugu wasaidie, je kama mtu hana ndugu atasaidiwa na nani? Na kama mtu anandugu na hawana uwezo wa kumsaidia afanyeje? Rejea maneno ya Kingmairo hapo juu, amesema kweli kabisa, yawezekana wewe umetoka familia yenye uwezo na mkopo kwako ni ziada tu, labda uliomba kwa kuwa uliona watu wanaomba.

Hivi unajua kuwa kuna wanafunzi wanaotegemea pesa ya meals and accommodation kulipa kiasi kikubwa cha ada ambacho bodi ya mikopo hailipi? Na je kila mtu akiamua kwenda kufanya field kwao, ili bsai hao ndugu wamsaidie, vipi kuhusu watanzania wengine wenye kuhitaji msaada wa vijana hawa watapataje? Lakini hata hivyo wanafunzi wa vyuo vikuu sio watoto wadogo, wanajua namna ya kupangilia bajeti zao, sio wote wasiojitambua, kwa hiyo fikiria tena ndo uandike vitu vinavyoeleweka.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu unavyoandika ufikirie kidogo, kumbuka hiyo pesa sio kila mtu anaitumia kwa anasa kama unavyodhani. Umesema ndugu wasaidie, je kama mtu hana ndugu atasaidiwa na nani? Na kama mtu anandugu na hawana uwezo wa kumsaidia afanyeje? Rejea maneno ya Kingmairo hapo juu, amesema kweli kabisa, yawezekana wewe umetoka familia yenye uwezo na mkopo kwako ni ziada tu, labda uliomba kwa kuwa uliona watu wanaomba.

Hivi unajua kuwa kuna wanafunzi wanaotegemea pesa ya meals and accommodation kulipa kiasi kikubwa cha ada ambacho bodi ya mikopo hailipi? Na je kila mtu akiamua kwenda kufanya field kwao, ili bsai hao ndugu wamsaidie, vipi kuhusu watanzania wengine wenye kuhitaji msaada wa vijana hawa watapataje? Lakini hata hivyo wanafunzi wa vyuo vikuu sio watoto wadogo, wanajua namna ya kupangilia bajeti zao, sio wote wasiojitambua, kwa hiyo fikiria tena ndo uandike vitu vinavyoeleweka.
 
Last edited by a moderator:
Kaka kwani hayo mahesabu unayopiga ni ndani ya kipindi hicho cha miezi hyo miwili,je hizi wiki tatu tangu hyo miezi miwili iishe unaizungumziaje ?

Halafu niulize hata km m2 ana matumizi mabovu kiasi gani ndo akicheleweshewa pesa asilalamike" m2 amalize mapema,aweke akiba hayo ni maisha binafsi ya m2 cha msingi kila mtu ana malengo yake over!
 
"Ukiwa una uhakika mchana utakula asbh kiporo unaweza kumwaga" hii ndo ilowakuta wanafunzi baada ya kujia hela ya field ipo wakatumia iliyokuwepo

Japo nao wanamakosa lakini hebu turudi kwenye ukweli nchi haiwezi kukosa pesa lijue hilo make BUNGE LA KATIBA linaanza ndo utajua hela ipo au la.na kama ni hvo mbona vyuo vingne wamepewa?

HII NDO TANZANIA.
 
Pesa ya boom ndogo sana kwa maisha ya sasa kaka...maana wengine tunapanga hatukai hosteli mfano vyuo vya private life gumu room ya kawaida kwa mwezi35000, umeme bado, maji bado mara, chakula bado utatoka kweli kiukweli life gumu huku field
 
Maandishi haya kijana ata kama utanyimwa hiyo hela utajua jinsi ya kujitetea ? Mara nyingi watoto wa maskini wanambwembwe sana.

Billy sawa nmekosea kutumia m2 badala ya mtu lakini point ya msingi ipo na imeeleweka
 
Nidhamu katika matumizi ya hela yapaswa iingizwe kwenye mitaala ya shule za Secondary.....hatuwezi kuwa na vijana wanaonua Kulalamika tu bila kuwa na Alternative solutions.
Kuna idadi Kubwa tu ya wanafunzi wanalipa cash vyuoni na siyo kwamba wanatoka Familia bora.
Kuweni wavumilivu as mpo TZ isiyokuwa na vipaumbele
Billy sawa nmekosea kutumia m2 badala ya mtu lakini point ya msingi ipo na imeeleweka
 
mkuu Excel nimejaribu kufikiria unatetea nini kwenye hoja zako nimekuta kwamba unatoa rai zako kwenye thread isiyotangamana na hoja zako.

Suala hapa ni kwanini serikali icheleweshe hizo pesa za wanafunzi? Je mkataba wao na loan board unasemaje? Kuna vitu vya kuwekea siasa ila sio jambo hili. Kama wanafunzi wana matumizi mabaya hayo ni mambo yao binafsi ila sio kigezo cha kuchelewesha pesa wiki tatu na sasa nafikiri itakuwa inaelekea ya nne.

Kwa matumizi ya kujibana kiasi gani mpaka mtu atumie laki nne na nusu kwa miezi mi3 kwa maisha ya changamoto za vyuoni? Mbona watu mnapenda sana kutetea maovu na uzembe wa serikali hii? Ningekubaliana nawewe kama pesa ingetolewa kwa wakati na malalamiko yaendelee kuwepo.

Tanzania ni zaidi ya tuijuavyo jamani, watu wana maisha magumu sana. Pitapita maeneo mbalimbali ya nchi hii utajionea mambo mengi ya kutisha kwenye maisha haya. Sasa wewe kama familia yako ina uwezo flani usiwadharau wala kuwahukumu wasio na uwezo.

Umesema wanaishi kwa starehe, sawa; ulitaka kuwapangia bajeti wewe? Au serikali kuchelewesha pesa zao inawasaidia nini kama sio kuwatesa tu? Wanafunzi wametukopa pesa mara mbilimbili huku wakitegemea pesa iingie ndio walipe.

Mama ntilie wanalalamika madeni ya wanachuo yamekuwa makubwa na wana wasiwasi kama watalipwa au la. Wanafunzi wanashinda njaa vujijivi huko hawana msaada wowote alafu mtu anakuta kutetea na hoja zake zinazoenda nje ya tatizo lililopo.

Tuwashauri serikali wawaonee huruma hawa wanafunzi. Wawapatie pesa yao haraka sana kwani hali ni mbaya. Tusitegemee ufanisi kwenye mafunzo ya vittendo wanayofanya kama wataendelea kuwa na njaa hii.

Hili ni bomu kubwa serikali inalitengeneza.
Kama kuna typing error mtanisamehe nimeandika nikiwa na jazba sana kwa kitendo hiki cha serikali hii zembe.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…