Mkuu EXCEl: ukipewa laki nne na nusu kwa miezi miwili na ushee utabakisha kias gan?. Udsm( mabibo hostel), nauli to and fro tsh.800, brk fast 1500, lnch 2000, dinner 2000, maji (mchna na jion) 1200, sabuni, vocha atlst 1000 per 2dyz, pango 750 per day, bado hpo crdb wananakato yao. Kumbka loan bord wanatoa 75000 for meals and accmdtion kwa siku 1 ambyo n sawa na lak 4 na nusu kwa miezi miwili yenye jumla ya siku 60, je n vp kwa miezi miwil yenye cku 61?. Kimsingi pesa kwa ajili ya meals na accomodation haitsh hta kidogo ss iv gharama za maisha zimepnda tofaut na miaka ya nyuma jamani.
Mkuu umetisha! yani chakula cha asubuhi unakula 1500? ni nini hicho we mwanafunzi unakula? unafanya kazi TRA mkuu?
lunch 2000 na dinner 2000? maji mchana na jioni 1200, hapa ongezea na 1500 ya BF jumla
7700!
Mkuu mbona una matumizi mabovu hivi kwa kulisha tumbo lako? kwani lazima ushushie soda na juice kila siku?
Vyakula vingi sidhani kama kuna kinachovuka shs 1500 kwa lunch and dinner kwa wanafunzi.. wewe naona umeamua kuongeza cost hewa tu hapa..
Hizo vocha unazoweka zilipangwa na serikali mkuu? hebu tuwe wawazi, kuna matumizi mengine tunayaweka kiasi kwamba tunajiumiza wenyewe...
Transport cost inategemea na wewe unaishi wapi, hiyo sikatai inaweza fika mpaka 800 ama kuzidi kwa siku..
Lakini tuseme ukweli, shs 7500 kwa ajili ya mlo na malazi hazitoshi kweli?
umepewa shs 2500 ambayo ni sawa na shs 75000 kwa mwezi kwa ajili ya malazi, kuna chumba kinazidi hiyo bei hapa mjini kwa mwanafunzi? kama kuna mazidi, kwanini msichangie muishi wawili?...
shs 5000 kwa ajili ya chakula.. 1000 asubuhi, 1500 mchana na 1500 usiku, baki 1000 ya ziada kwa maji nk,
serikali sidhani kama itapiga mahesabu ya kukupa surplus hata siku moja..
Mkuu, wanafunzi wa vyuo tuna matumizi ya pesa mpaka sehem zisizohusika.. CLUB ni sisi, BEACH kila weekend ni sisi, BASH za hapa na pale ni sisi... kwa hiyo hiyo 7500! lazima tutalia njaa tu!