Fedha zilizotengwa kwaajili ya maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru, kutumika kununua vifaa vya Hospitali ya Uhuru Jijini Dodoma

Fedha zilizotengwa kwaajili ya maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru, kutumika kununua vifaa vya Hospitali ya Uhuru Jijini Dodoma

Faith Luvanga

Member
Joined
Aug 21, 2018
Posts
14
Reaction score
15
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza shilingi milioni 835,498,700 zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya shamrashamra za sherehe za maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Tanzania Bara, Desemba 9, 2020 zitumike katika kununulia vifaa mbalimbali kwa ajili ya Hospitali ya Uhuru ambayo kwa sasa ujenzi wake umefikia asilimia 92 na inatarajiwa kufunguliwa Desemba 30 mwaka huu.

Rais Dkt. Magufuli ameagiza siku hiyo itumike kwa ajili ya kufanya shughuli mbalimbali za kijamii nchini.

Kauli mbiu ya maazimisho ya 59 ya Uhuru wa Tanzania Bara kwa mwaka huu inasema; ‘Miaka 59 ya Uhuru na Miaka 58 ya Jamhuri: Tanzania yenye Uchumi Imara Itajengwa na Watanzania Wenyewe, Tufanye Kazi kwa Bidii, Uwajibikaji na Uadilifu.’

Pia, Soma: Dar: Yaliyojiri Maadhimisho ya Miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika Uwanja wa Uhuru

09 Dec, 2019: Maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru wa Tanganyika. Wafungwa 5,533 wapata msamaha wa Rais. Mbowe ataka maridhiano ya Kitaifa
 
Waseme tu ukweli, pesa za ndani hakuna, na pesa za mabeberu nazo zimekuwa za kuwindwa na manati.
Vyuma vimekazaaaa.
Kwa sisi wapenzi wa paredi tumeridhika kwa vile tarehe 4-6/11/2020 tulishuhudia vitu adimu kutoka kwa vijana wetu.
na sio mbali toka tuone status ya utayari kwa BARA NA VISIWANI.
so acha maendeleo ya kazi yaendelee.
 
Kukikaribia ndo vijisababu ndiiii

Sema pesa zimeishia kwenye kampeni


Yaani ocean road dawa hamna ila mwezi wa saratani walijinadi na kuwasema wagonjwa wanakimbilia miti shamba kumbe unafki tu.


Hiyo hospital ya Uhuru watainunulia vifaa vipi ile ya mtwara?


Unafki mwingi
 
Mdee njoo Chadema upate na mimba sasa.
 
Taarifa kutoka kwa waziri mkuu mh Majaliwa zimehabarisha kuwa sherehe za miaka 59 ya Uhuru zimeahirishwa.

Badala yake watu watafanya Huduma za kijamii kila mtu katika eneo lake na fedha zilizotengwa kwa sherehe hizo takribani Ths. 800 milioni zitatumika kununulia vifaa vya hospitali ya Uhuru.

Source: Eatv habari
 
Back
Top Bottom