Fedha zilizotumika sherehe za kuadhimisha Miaka 45 ya CCM zingeelekezwa kwenye huduma za jamii

Fedha zilizotumika sherehe za kuadhimisha Miaka 45 ya CCM zingeelekezwa kwenye huduma za jamii

Koryo2

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
2,056
Reaction score
2,519
Kwanza kabisa niipongeze Chama cha Mapinduzi kufanya sherehe yake ya miaka 45 Mkoani Mara katika Manispaa ya Musoma.

Najua kuwa rasilmali nyingi zimetumika lakini ni matumizi ya siku moja tu LAKINI kwa ushauri wangu rasilmali zilizotumika leo zingeelekezwa katika miradi ya maendeleo kama barabara, Vituo vya Afya, kununua magari ya wagonjwa nk.

Hapa ndo bado namkumbuka Marehemu Mhe. Dr. Magufuli mawazo yake yangekuwa tofauti na mawazo ya leo.
 
KWANI CHADEMA MMENYIMWA KUAZIMISHA BIRTHDAY YA CHAMA CHENU
 
Pesa za umma zinapigwa na sisi tunashangilia, kwa ujinga huu umasikini Tz ni wa milele
 
Unataka kuniambia walinzi wa Rais wanalipwa na CCM leo? shame on you
Hao walinzi wanamlinda mkuu wa nchi hapo ambaye ni mwenyekiti wa Ccm....sasa tatizo lipo wapi hapo?
 
Hapa ndo bado namkumbuka Marehemu Mhe. Dr. Magufuli
Utamkumbuka Sana tu. Na ikibidi utaanza kumuota,lkn ukweli mchungu ni kwamba hafufuki tena hivyo hatorudi. Yuko zake motoni anaungua kwa maovu aliyoyatenda.
 
Unaweza kuwa na point nzuri.Ufujaji wa fedha hapa nchini ni kitu cha kawaida sana.Wakati tukiwa hatuna vituo vya afya,magari ya wagonjwa ama ukosefu wa madarasa ya shule tulikuwa tunanunua maV8 kwa maelfu kila mwaka kwa ajili ya viongozi.

Wakati tunaanza ujenzi wa bomba la gas asilia toka Mtwara tulikataa kujenga mitambo ya kufua umeme kule kule Mtwara na kusafirisha umeme toka huko.Badala ya kusimika mitambo ya kufua umeme pale Kinyerezi tukapeleka matrilioni ya fedha Rufiji.

Mifano ya ufujaji wa raslimali zake mwingine ni kujenga reli ya SG ya umeme kwa njia ya kati kabla ya kujenga reli ya Mtwara hadi Mbamba Bay au kuboresha TAZARA na TRC.

Orodha ni ndefu na ukiwaza yote unahitimisha kuwa Tanzania chini za CCM na katiba ya 1977 imekwama-Sturked headon in Mud.
 
Utamkumbuka Sana tu. Na ikibidi utaanza kumuota,lkn ukweli mchungu ni kwamba hafufuki tena hivyo hatorudi. Yuko zake moyoni anaungua kwa maovu aliyoyatenda.
Nakuapia magufuru hawezi kuwa motoni,,hizo ni lugha za watu wasio na dini au dini uchwara.Hawa unaowaona ni wa maana basi ndo utawakuta motoni.Magufuru alipata mda wa kutubu ambayo ni bahati kwa wachache
 
Unataka kuniambia walinzi wa Rais wanalipwa na CCM leo? shame on you
Hiyo ni fixed cost Mkuu.
Au unataka kutuambia mishahara ya walinzi wa Rais itakuwa na nyongeza y siku moja waliomlinda Rais akiwa kwenye sherehe ya Chama chake?


Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Kwanza kabisa niipongeze Chama cha Mapinduzi kufanya sherehe yake ya miaka 45 Mkoani Mara katika Manispaa ya Musoma...
hapo niwatetee, ccm ina miradi mingi sana, na pesa nyingi sana. unataka watumie fedha za chama kwenye miradi? wawe wanatoa kama msaada au nini, manake kwenye hiyo miradi kuna pesa za taifa ambazo ziko kwenye bajeti.

ukiend akila mkoa hawa jamaa wana majengo na maduka na vitega uchumi vingi, pesa wanazo nyingi sana. ni za kwao bila kushare na chama wala taifa.
 
Back
Top Bottom