Fei Toto aliomba kuvunja mkataba baada ya kuchoka manyanyaso

TFF haina mamulaka ya kuvunja mkataba unataka wafanyeje? na kama anaona hatendewi haki aende mbele
 
Hahaha Fei ashikilie hapo hapo. Bora kuanza kuuza mishkaki mapema kuliko kuuza baada ya kustaafu soka.
 
Huyo mtoto hajui kusoma alama za nyakati huu utawala mama si wa magu naishia hapo .hawezi pambana na viongozi wa yanga
 
Inapwaya vip ndugu yetu mwambie alete pesa
 
Nilicho shangaa Leo ni msimamizi wa Feitoto Dada Jasmin kushangaa kamati ya Haki na Hadhi za wachezaji kuwa kama mahakama.
Sasa kama FIFA wana CAS ambayo ni mahakama kamili ya kutatua migogoro inakuaje FA za nchi ambazo zinafuata structure ya FIFA zikose kamati za kutatua migogoro katika mpira!!
Kamati ya Haki na Hadhi za wachezaji ni mahakama ya soka Tanzania.
Ndiomaana Members wa kamati ni Wana Sheria na wapo ambao si wanasheria.

Ata mahakama zetu zina wanasheria lakini wapo wazee wa Baraza wengi hawajasoma Sheria ila wanauzoefu na busara.
Iyo Kamati imesha fungia wachezaji, Makocha watu binafsi n.k ni mahakama kamili ya soka.
 
At the end of the day , all of them might end loosing. Thamani ya mchezaji inazidi kupungua kila siku na quality ya mchezaji inapungua vilevile. Just get over it and stop being big headed. We all learn through mistakes.
 
Mkuu TFF sio kama mahakama, bali ni mahakama. Na ndio maana unaona inafungia wachezaji, makocha na waamuzi. Ishu za mpira wa mguu zote zinashughulikiwa na TFF. Ukiona haujaridhika ndio unakata rufaa unaenda ngazi ya juu zaidi ambayo ni CAS.
Point yangu kusema hivyo ni kuwa TFF kwa kesi hii ni msuluhishi siyo mahakama anayeenda kumjadili mtuhumiwa na kumuhukumu.

Kwa hivyo, wanapotoa mwezi wa kujiandaa kwa kikao kijacho, nategemea pande zote zinakuwa zinawasiliana na TFF kwa kipindi hicho ili muda wa kikao ukifika mambo ya msingi yanakuwa clear na upenyo wa kuleta mapingamizi kama walivyofanya jana Yanga hauwezi kuwepo, at least siyo mwanzoni tu wa kikao.

Inaonyesha kama msuluhishi, TFF haikuwa imefanya kazi yake kipindi hiki chote kujiandaa na kikao husika.
 
TFF haina mamulaka ya kuvunja mkataba unataka wafanyeje? na kama anaona hatendewi haki aende mbele
Wanashindwa kufanya jukumu lao kutolea ufafanuzi au tafsiri ya mkataba kati ya mchezaji na timu. Naamini hilo liko ndani ya uwezo na majukumu yao.

Kwa nini baada ya kusoma mkataba wasimwambie kwa mujibu wa mkataba huu, Feisal ili kuuvunja mkataba huu unasema fanya hivi na hivi. Kama alifanya makosa hapo nyuma ya kuvunja bila kufuata taratibu, ili kuuvunja mkataba na kwa kuzingatia makosa hayo (TFF pia wakiwasiliana na Yanga juu ya hilo maana ni wazi Feisal hataki kufanya mawasiliano yoyote tena ya moja kwa moja na Yanga), adhabu yake ni hii na hii, lipa tumikia adhabu hii uwe huru.

TFF ni mlezi na msimamizi wa mpira, wasikwepe majukumu yao kama wasuluhishi wa migogoro.
 
Let us assume wewe ndo Kiongozi wa ngazi za juu wa yanga... Hicho kitu ungekiruhusu?
 
Nyie ndo mmempoteza dogo. Mlijua tff itaamua kama mnavyotaka nyie ili mlipe faini kijana awe huru mmchukue.

Kwa akili yako unadhani tff hawajui huo mtego mlioweka.

Hebu nendeni mezani Yanga ukapewe thamani yake mlipe au ka vip msubiri mkataba wake uishe mmchukue for free.
 
We bwana si uende CAS mkapewe haki yenu mnayodai, kwan shida nin hasa?!
 
Yanga kabakisha step kadhaa kucheza fainali. Laiti kama Yanga itacheza fainali ya CAF confederation msimu huu, Feitoto atakuwa na historia mbaya sana ya kusimulia kwenye carrier yake ya mpira.
 
Yanga kabakisha step kadhaa kucheza fainali. Laiti kama Yanga itacheza fainali ya CAF confederation msimu huu, Feitoto atakuwa na historia mbaya sana ya kusimulia kwenye carrier yake ya mpira.
mpaka hapo walipofikia tayari ana historia mbaya ya kusimulia hatocheza mpira tena afikie nusu fainali
 
mpaka hapo walipofikia tayari ana historia mbaya ya kusimulia hatocheza mpira tena afikie nusu fainali
Kabisa, ila fainali itakuwa ni nzuri zaidi maana atakuwa anawashuhudia wenzie wakiwa wanavishwa medali kwa tv
 
Hukuna mutual agreement kama pande mbili hazikai meza moja. Nadhani mwajiri kamwambia wakae mezani ila Fei na mawakili wake wamekataa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…