Fei Toto aliomba kuvunja mkataba baada ya kuchoka manyanyaso

Fei Toto aliomba kuvunja mkataba baada ya kuchoka manyanyaso

View attachment 2585280

Aliandika kwa TFF kwamba alichoka manyanyaso mbalimbali kutoka kwa uongozi. Ni mambo ya kusikitisha
Hayo manyanyaso ni ya aina gani? Na kabla ya kufikia hiyo hatua ya kubunja mkataba, alishtaki kwenye vyombo gani vya kisheria, ili kuondakana nayo?

Kwa nini asinyooshe tu maelezo yake ya kurubuniwa na wajanja wa mjini, na mwisho wa siku kuangukia pua?
 
Hii nchi na nchi nyingi za Africa zimechelewa na huenda hazitakuja kuendelea Kwa sababu kuu moja "kutokufuata Sheria"

Labda wengi wanaomsapoti Fei na kuona kama Yanga inamnyanyasa au kumkoa ni mashabiki wa Simba hivo wanaongea tu kishabiki lakini hua najiuliza wapo serious? Mwingine utakuta mishipa imemsimama kua "kwanini yanga mnng'ang'ania Fei wakati Fei mwenyewe haitaki Yanga?!" Nabaki nacheka tu.

Kwanza Yanga haiwezi kumbania Fei na wala haina hiyo Nia ndio maana wakasema kama ni kuvunja mkataba aende kilabuni wavunje au kama kuna timu inamtaka iende ofisini.

Lakini bado kuna watu wanaona kama Yanga ndo wabaya Hadi nashangaa. Eti itumike busara tu.. busara???
Leo Kwa Fei itumike busara kesho Mayele nae aingie vichochoroni keshokutwa Mauya, mara Aucho au Job hivi nini maana ya mkataba???

Kama ni hivo sioni haja ya kua na mkataba sasa [emoji16]
 
Yanga wanamfanyia utu sana sababu wamemlea na wanamjali.
Ameshakua kajazwa ujinga na wasiomtakia mema waliodhani wataidhoofisha Yanga, wakamfundisha hadi kuichukia Yanga, na akamtanguliza hadi mama yake mbele ili tu wafanikishe kujenga chuki.
Huyu si wa kuhurumiwa tena, wakamatie hapohapo...Mchezaji wa Zenji kabisa huyo.
Mwingine huyu
 
Image ya Yanga inapwaya kwa kufuata sheria na taratibu za soka?

Image inapwaya kwa kumuadabisha mchezaji mtovu wa nidhamu?

Acheni ushabiki maandazi hakuna huruma kwenye sheria. Imagine ingekua Yanga ndio ka mis behave kwa dogo mngesema ivyo ivyo dogo aionee huruma Yanga?
Huyu ndo kabisaa
 
Huyu ndo kabisaa
Bush lawyer unakula za uso daily. Mtetezi wa haki za binadamu unaangukia pua
JamiiForums-192276710.jpg
 
Mwanzoni mwa huu mgogoro Mwenyekiti wa kamati ya Haki na Hadhi za wachezaji alisema, Wakati wanasikiliza shauri Kwa mara ya kwanza Mawakili wa Yanga walitaka mchezaji aileze kamati Sababu ya Kuvunja mkataba.
Afafanue manyanyaso aliyokua akifanyiwa na Yanga labda yanaweza kuwa na mantiki.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti, Mawakili wa Feitoto walikataa Fei Toto kueleza mbele ya shauri ilo Sababu za Kuvunja mkataba ila kikao kielewe mchezaji hajaridhika na mazingira ya kazi yake.
Kamati ikawaeleza Mawakili wa Feitoto basi baada ya hoja za pandembili kusikilizwa, Watamuita Fei Toto chemba na kumsikiliza ila maelezo atakayo yatoa hayata tumika kama kielelezo Cha kesi.

Mawakili wa pande zote wakakubaliana na hoja iyo.
Kamati ilimsikiliza na Mwishowe wakatoa maamuzi Waliyo yatoa.

Kwasasa Feitoto Hana hoja mpya ya Msingi na Kamati ndio ileile na majibu yatakua ndio yaleyale kwakua hoja za Kuvunja mkataba ndio zilezile.

Kama anaona anaonewa aende CAS akutane na maamuzi ya kibabe na ya kushurutishwa kuliko Aya ya Tff.
Hivi unaelewa kwann mahakamani kesi hua zinatupwa na kurejeshwa upya ,hujui
 
Bro, unajidhalilisha kuandika haya bila kuyataja hayo manyanyaso anayopata toka kwa viongozi wa Yanga. Hivi tarehe ya barua haikuambii kitu chochote..!???

Kifupi Fei toto kachemsha Big time, na waliokuwa wanampa kichwa wamemuacha peke yake
He is alone without any support from wachawi FC,[emoji24][emoji24][emoji24]kinachomdhalilisha ni Yanga kuendelea kufanya vizuri bila yeye [emoji137][emoji137]
 
TFF wanakosea wanapojaribu kuendesha hii ishu kama vile wao ni mahakama. Inakuwaje mnawapa pande mbili zaidi ya mwezi kujiandaa kwa mashauri halafu siku ya kukutana mnaanza tu kikao, upande mmoja unatoa mapingamizi yanayolazimu kikao kuahirishwa. Mwezi wote huo pande zote na TFF walikuwa wanafanya nini?

Wanachofanya Yanga ni kumkomoa tu Feisal na kucheza delaying tactics na wanafanya hivyo kwa sababu wanajua ana haki ya kufanya anachofanya.
 
He is alone without any support from wachawi FC,[emoji24][emoji24][emoji24]kinachomdhalilisha ni Yanga kuendelea kufanya vizuri bila yeye [emoji137][emoji137]
Kwasasa anaona aibu sana, na ndio maana hatamani hata kurudi Yanga tena. Alijazwa sifa, ya kuonekana Yanga bila Feisal hakuna kitu. Kajazwa maneno kuwa yeye ndiye anayeibeba timu kwa mabega yake. Basi na yeye akayasikiliza maneno na kuvimba. Siku Yanga amefungwa goli mbili na Monastir akapost anaonesha matokeo ya mechi kwenye simu yake huku akijawa na furaha kwa kicheko. Ila kwasasa yeye ndio anaonekana hana faida timu bado ipo kwenye malengo yaliyojiwekea na uwanjani mpira unachezwa vizuri kabisa bila kuonekana kuna pengo la mtu.
Huko alipo apige dua na maombi Yanga isifike fainali, kama ikitokea imefika fainali basi atakuwa na historia mbaya sana ya kusimulia wanae huko mbeleni kwa uzuzu aliouonesha.
 
TFF wanakosea wanapojaribu kuendesha hii ishu kama vile wao ni mahakama.

Mkuu TFF sio kama mahakama, bali ni mahakama. Na ndio maana unaona inafungia wachezaji, makocha na waamuzi. Ishu za mpira wa mguu zote zinashughulikiwa na TFF. Ukiona haujaridhika ndio unakata rufaa unaenda ngazi ya juu zaidi ambayo ni CAS.
 
Back
Top Bottom