Mkuu haya mambo yanavyozidi kusambaa Image ya Yanga huku nje inapwaya kuliko ya Fei, narudia tena Club kubwa kama Yanga ni kuachana na hili jambo haraka - Yanga ni bland na kuzidi kuwa kwenye media kila siku kwa shutuma kama hizi si jambo nzuri.Mkuu wewe ndiye unayeleta ushabiki, unataka Yanga watumie huruma ili wachezaji wengine wajifunze kitu gani?
Feisal hajakatazwa kuondoka bali Yanga hawapo tayari kuondoka kiuhuni, kama Yanga itaruhusu huo upuuzi ina maana itakuwa ni taasisi ya kihuni.
Na la mwisho Feisal kaisha ichafua taasisi kwa kusema kuwa alikuwa ananyanyaswa, lazima aoneshe ushahidi na maelezo ni kwa yapi alikuwa ana nyanyaswa.
Kwa sakata hili Yanga inapoteza zaidi kuliko Fei nakuhakikishia.