FEI TOTO NA KADI ZA NJANO

FEI TOTO NA KADI ZA NJANO

marcoveratti

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2017
Posts
1,019
Reaction score
1,824
Feisal Salim 'Feitoto' ... Kwa takwimu Msimu huu pekee ameshapata kadi 15 za njano. .
.
Aliukosa mchezo wa ugenini dhidi ya Mtibwa kwa kosa la kua na kadi 3 za njano mfululizo. .
.
Mchezo aliorejea dhidi ya Azam, alipata kadi, mchezo uliofata tena dhidi ya Prison, amepata tena kadi ya njano, hivyo kama atapata kadi tena mchezo ujao, atakosa mchezo mmoja. .
.
Nini shida kwa FeiToto? Wengi wamekua wakijiuliza hili.

Binafsi nafikiri majukumu mapya aliyonayo kwenye mbinu za Mwinyi Zahera yamekua yakiinufaisha Yanga kwa maana ya kiuchezaji lakini yamemuathiri sana Fei. Kivipi?

Fei anacheza kwenye role ya kiungo wa Ulinzi akiwa na jukumu la kuichezesha timu kutokea pale. Kitaalam anaitwa deep lying playmaker. Kule Italia anafahamika kama "Regista".
.
.
Licha ya uwezo mkubwa wa kupiga pasi fupi na ndefu, kontroo ya mpira, kiungo wa eneo hilo anatakiwa pia awe na uwezo wa kupokonya mipira.
Ni kama alivyokua Xabi Alonso. Ni kama alivyo Marco Verrati.
.
.
Feitoto amefanikiwa kuichezesha timu lakini hana sifa ya mwisho inayohitajika kwenye eneo hilo. Kupokonya mpira bila kucheza rafu. Hawezi kufanya Clean tackle. Hajazoea kwenye makuzi yake kazi hiyo...
Unadhani Zahera afanye nini kumnusuru Fei toto na kadi za njano.....
IMG_20190503_135151_891.jpeg
 
Mkuu huyu mtoto tu wakati mwingine miyeyusho anacheza faulo zisizo na msingi..
Mchunguze fei utakuja gundua hili, wakat mwingine nahisi aidha ni utoto ama ana tabia binafsi mbovu kwamba kashajiona yeye ndio yeye, wakat mwingine akiporwa mpira anakuwa mtata wakati mwingine anacheza rafu pasipo mpira, kukoromeana koromeana hovyo..

Pirlo alikuwa anacheza nafasi hyo ila hakuwa mtu wa kuzikoga kadi hovyo
 
Kiungo mkabaji ukiogopa kadi ya njano umefelisha... Ni namba inayoongoza kwa kupewa kadi za njano,.. Kawaida tu
 
Leave him alone. With time, hizo yellow cards zitapungua kulingana na majukumu anayopewa na uzoefu anaopata.

Angalia Ninja ana improve kila siku. Yellow na red cards zimepungua. Faulo ndani ya penalt box zimepungua sana.
 
Mkuu huyu mtoto tu wakati mwingine miyeyusho anacheza faulo zisizo na msingi..
Mchunguze fei utakuja gundua hili, wakat mwingine nahisi aidha ni utoto ama ana tabia binafsi mbovu kwamba kashajiona yeye ndio yeye, wakat mwingine akiporwa mpira anakuwa mtata wakati mwingine anacheza rafu pasipo mpira, kukoromeana koromeana hovyo..

Pirlo alikuwa anacheza nafasi hyo ila hakuwa mtu wa kuzikoga kadi hovyo
Sawa kabisa Mkuu,Kadi nyingi za Toto ni uzembe na utoto mwingi,utakuta anapewa Kadi bila hata kuwa na mpira au kukabana na Mchezaji.
 
Feisal Salim 'Feitoto' ... Kwa takwimu Msimu huu pekee ameshapata kadi 15 za njano. .
.
Aliukosa mchezo wa ugenini dhidi ya Mtibwa kwa kosa la kua na kadi 3 za njano mfululizo. .
.
Mchezo aliorejea dhidi ya Azam, alipata kadi, mchezo uliofata tena dhidi ya Prison, amepata tena kadi ya njano, hivyo kama atapata kadi tena mchezo ujao, atakosa mchezo mmoja. .
.
Nini shida kwa FeiToto? Wengi wamekua wakijiuliza hili.

Binafsi nafikiri majukumu mapya aliyonayo kwenye mbinu za Mwinyi Zahera yamekua yakiinufaisha Yanga kwa maana ya kiuchezaji lakini yamemuathiri sana Fei. Kivipi?

Fei anacheza kwenye role ya kiungo wa Ulinzi akiwa na jukumu la kuichezesha timu kutokea pale. Kitaalam anaitwa deep lying playmaker. Kule Italia anafahamika kama "Regista".
.
.
Licha ya uwezo mkubwa wa kupiga pasi fupi na ndefu, kontroo ya mpira, kiungo wa eneo hilo anatakiwa pia awe na uwezo wa kupokonya mipira.
Ni kama alivyokua Xabi Alonso. Ni kama alivyo Marco Verrati.
.
.
Feitoto amefanikiwa kuichezesha timu lakini hana sifa ya mwisho inayohitajika kwenye eneo hilo. Kupokonya mpira bila kucheza rafu. Hawezi kufanya Clean tackle. Hajazoea kwenye makuzi yake kazi hiyo...
Unadhani Zahera afanye nini kumnusuru Fei toto na kadi za njano.....
View attachment 1087005
Bagi alizofundishwa kuvuta pale Yanga ndo zinamwathiri
 
Marefa ndio tatizo..tackle za kawaida Bongo yellow card..wanafikiri mpira ni kucheza blues. .
 
Back
Top Bottom