Ilianza km utani utani vile na sasa ni dhahili.Azam wakiamua hakuna wa kuwazuia si Simba wala Yanga. Waliwahi fanya hivyo kwa Ngasa na sasa wamefanya kwa Fei.
Binafsi mimi ni shabiki wa Yanga ila nampongeza sana Fei kwa maamuzi aliyochukua. Nasikia Azam watampa mshahara mara 3 ya ule aliokuwa anapata Yanga. Maana yake atapata zaidi ya mil.15.Na hii iwe fundisho kwa viongozi wa Simba na Yanga kuacha kuwadharau wachezaji wa ndani. Inakuaje mchezaji km Fei unamlipa Mil.5 wakati akina Aziz Ki wanachukua dola elfu 8?
Mchezaji akiomba kuongezewa pesa anapewa majibu ya ovyo. Haiwezekani wachezaji wa kigeni wenye viwango vya kawaida kulipwa mamilioni ya pesa (15-20) aafu wachezaji wetu wa ndani wenye uwezo zaidi ya hao tena wafia timu wakilipwa milion(5 -7). Hebu angalia kwa mfano pale Simba wachezaji km Kapombe, Zimbwe jr,Mzamiru si ajabu kukuta wanazidiwa mbali sana na akina Onyango,Okwa,na Okra.
Tabia ya kudharau wachezaji wetu wa ndani imehamia hadi kwetu mashabiki. Yaani akikosea Morrison,au Mayele ni sawa,no one cares. Ila akikosea Kibu Denis au Mkude mashabiki watatukana mpaka Saikolojia ya mchezaji inaathirika. Tunadharau sana vyakwetu sijui na katuroga!
Asante sana Fei kwa maamuzi yako hakika utawaamsha wenzako waliolala kwenye usingizi wa fofofo wakimezwa na sifa za Simba na Yanga. Samata alikimbia utumwa wa Simba na Yanga na sasa ni tajiri, muhimu ni unga wa familia yako. All the best wish to see you in mwananchi jersey one day.[emoji122][emoji122][emoji122]