Kinumbo
JF-Expert Member
- Dec 8, 2019
- 3,039
- 5,560
Fact kubwa sana hii, binafsi mimi sina Usimba na Uyanga wala soka la Bongo silifuatilii kabisa. Ila kwa wachezaji ninao wakubali hapa nyumbani ni Aishi Manula na Fei Toto. Huyu Fei kwa alipo fikia hakupaswa kucheza kwa ligi ya nyumbani tena, alipaswa kutoka. Hapo nyuma nilisikia kuna klabu kutoka Uarabuni huko ilikuwa inahitaji huduma yake sijajua nini kilitokea. Wakala wa Fei inaonekana ni kilaza sana
Hakuna timu ambayo inaua viwango vya wachezaji kama Azam fc! Timu ina kila kitu!
Viwanja vya mazoezi, gym, mabwawa ya kuogelea, nk lakimi ukiwakuta wachezaji karibia wote wana vitambi! Ni suala tu la muda, yule SOPU aliyetoka Coastal, atakuwa ni historia.
Kama Fei Toto ana akili, bora akaendelea tu kubakia kwenye klabu yake aliyo izoea. Na kama ni suala la maslahi, hilo ni jambo linalo zungumzika. Maana mchango wake kwenye timu unaonekana.
Na kama anataka kubadilisha mazingira, basi atafute timu za nje akacheze. Aache kufuata nyendo za wenzake kama Gadiel Michael na Ibrahim Ajib! Tangu waondoke Yanga kwa kisingizio cha maslahi, wanahangaika tu huko waliko.