Feisal Aje Yanga Tumalizane,Yanga ni kubwa kuliko Yeye

Feisal Aje Yanga Tumalizane,Yanga ni kubwa kuliko Yeye

Smart codetz

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2023
Posts
218
Reaction score
875
Tangazo la Yanga la March 6 ambalo lilikuwa very clear katika option ambazo tumetoa, tumesema kama Feisal anataka kuondoka aje Yanga aondoke kama Kuna klabu inamuhitaji aje klabuni tumpe mkono wa kwa heri.

“Hizi option zote anazozitafuta hapa tunashangaa kwanini yupo hapa, sisi sio kwamba tunamng’ang’ania Feisal mpaka ionekane tunamnyanyasa, hata leo akija klabuni pale akasema anataka kuondoka tunakaa nae mezani tunaachana nae.

“Ni kutunisha tu mabega yake Hakuna ugumu wowote kama angetaka kusave carrier yake sisi hatujamfanya kitu chochote, Feisal hajafukuzwa na Yanga yeye mwenyewe kaamua kufanya utoro kwa kuondoka kambini, hawezi kuwa mkubwa kuliko klabu na hatokaa awe mkubwa zaidi, Yanga ilikuwepo kabla hajazaliwa na itakuwepo hata asipokuwepo tena,” Mwanasheria wa Yanga Sc, Simon Patrick
5DE581B3-2E0E-4FA9-82A1-5C48811707CD.jpeg
 
Kuna hoja inaibuliwa kwamba yanga inamngangania Feisal. Nashangaa sana ni kwanini asiende pale jangwani akamalizane na yanga ilihali yanga haina ubaya wowote nae. Na wamemuita mara nyingi sana huyu dogo lkn hataki.

Hivi ni kitu gani kinamfanya asiende jangwani akamalizane nao? Anataka avunje mkataba juu juu kihuni kama uswahilini.
 
Feisal moyo wake upo Yanga ndio maana hataki kwenda Yanga ili wayamalize, ni sawa na mke anayetishia kuondoka alafu anaacho vilago vyake vyote ndani anachotaka abembelezwe ili abaki
 
Kuna hoja inaibuliwa kwamba yanga inamngangania Feisal. Nashangaa sana ni kwanini asiende pale jangwani akamalizane na yanga ilihali yanga haina ubaya wowote nae. Na wamemuita mara nyingi sana huyu dogo lkn hataki.

Hivi ni kitu gani kinamfanya asiende jangwani akamalizane nao? Anataka avunje mkataba juu juu kihuni kama uswahilini.
Akienda tu yanga ataambiwa alipe mil500
 
Kwenye hili sakata inabidi maamuzi yake yafanyike kwa umakini mkubwa. Vinginevyo TFF wasipokuwa makini kwenye maamuzi basi tutegemee vurugu kubwa kwenye soka letu na hasa itakuwa balaa kwenye hizi timu zetu kubwa tatu Yanga, Simba na Azam. Kwani timu mojawapo kati ya hizo ikimtamani mchezaji wa upande mwingine hata kama atakuwa na mkataba wa muda mrefu basi inazungumza na mchezaji inamrubuni wanampa pesa akavunje mkataba.

Kwa maana hiyo wale wote wanaoshabikia sakata hili na kudhani kuwa tu Yanga ndio itaathirika basi watakuwa hawaoni mbele na hawalitakii mema soka la nchi hii. Kwani likiruhusiwa hili la Fei Toto basi ndio itakuwa vigezo kwa hao vigogo watatu kuleta vurugu kwenye soka letu na vilabu vidogo ndio vitaumia zaidi na mwisho ligi yetu kukosa msisimko na ushindani.

Ni mtizamo tu.
 
Back
Top Bottom