BANDOKITITA
JF-Expert Member
- Oct 4, 2022
- 1,484
- 2,852
Kazumari kamwaga unyunyu jamani. Ebu tujadili huu mkataba wa Feisali.
Kwanza ni KWELI pasi na shaka yoyote kwamba Feitoto amewapa NOTISI klabu yake ya Yanga SC ya kuvunja mkataba nao.
Feisal alikuwa na mkataba na Yanga SC (ambao BIN KAZUMARI imeuona) uliosainiwa tarehe 10 Agosti 2020 ukichukua nafasi ya ule uliosainiwa 2018. Mkataba huu unamalizika tarehe 30 Mei 2024.
Kipengele cha 2.3 cha mkataba kinazungumzia pesa ya usajili ambayo ni Tshs 100,000,000/= kwa kipindi chote cha mkataba ambacho kimsingi ni miaka 4 (2020 - 2024).
Kama ilivyo mikataba mingi kwenye mkataba huu pia kuna vipengele vya KUVUNJA mkataba ambacho ni namba 14 (Expiry, suspension and termination of the contract).
Katika kipengele namba 14.7 kama kilivyonakiriwa kwenye barua (notisi) ya kuvunja mkataba (swipe left) kinampa haki mchezaji kuvunja mkataba katika hali isio ya kawaida kwa kulipa pesa ya usajili kama inavyoainishwa na kipengele cha 2.3 na walau mshahara wa miezi 3.
Ukisoma katika kipengele cha 5 kinachozungumzia mshara, bima na malipo/ada nyingine (salary, insurance and other fees ) utagundua kipengele cha 5.1 kinasema mshahara wake ni Tshs 4,000,000/= kwa mwezi. Kwa miezi 3 kama unataka kulipa manake ni Tshs 12,000,000/=
Hiyo ndiyo sababu ukisoma notisi ya kuvunja mkataba inasomeka kwamba Feisal AMEILIPA Yanga SC Tshs 112,000,000/= ili kuendana na takwa la kimkataba. Kwamba milioni 100 pesa ya usajili na milioni 12 mshahara miezi 3.
Kipengele cha 18 ambacho ni cha mwisho kabisa katika mkataba kinazungumzia UHAMISHO WA BAADAE (Future Transfers). Ambapo 18.1 imasema "Mchezaji anaweza kuhamishwa kwenda klabu nyingine kukiwa na haja hiyo. Klabu inaweza kuanzisha mazungumzo na kufanya jitihada zake zote kuhakikisha usajili huo unafanikiwa juu ya kwamba klabu itaweka na kuamua pesa ya uhamisho kuendana na soko la wakati huo ambayo haitokuwa chini ya dola za kimarekani laki moja isipokuwa ikiamuliwa vinginevyo na klabu,ada ya uhamisho iliyotajwa itajumuisha mazingatio ya mchezaji kuhamia klabu nyingine"
Baada ya Feisali KUVUNJA mkataba KULIPA na kutoa notisi anakua mchezaji huru anaeweza kujiunga na klabu yoyote kama hakuna kipengele kilichokiukwa. Kipengele cha 18.1 hakiwezi kumbana tena.
Kimsingi hii mikataba ya Bongo wachezaji wetu wengi wanapigwa sana. Ebu fikiria mtu kurudisha 100,000,000 na mishahara ya miezi 3 juu. Wakati huo kaichezea timu muda mrefu tena Kwa mafanikio. Kwa maisha ya Kibongo huu mimi naona ulikuwa mkataba wa kumbana hadi kuishiwa pumzi. Kwa ufupi ulikuwa mkataba wa kikatili na wa kipuuzi kabisa.
Hii mikataba mingine tuwaachie wazungu ambao bonus zao tu zinawatosha hata bila kugusa mshahara. Sio kukopi na kupesti Kila kitu.