Smart codetz
JF-Expert Member
- Jan 25, 2023
- 218
- 875
Feisal Salum “Feitoto” atinga tena TFF akiwa na aliyemsaidia Saimon Msuva kushinda kesi CAS. Mara hii amewasilisha barua ya maombi kwa TFF akitaka kuvunja mkataba wake na klabu yake ya YANGA
============
Mchezaji wa Klabu ya Yanga, Feisal Salum, Machi 6, 2023 amefika kwenye Ofisi za Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), Dar es Salaam kwa ajili ya kuwasilisha ombi kulitaka Shirikisho hilo kuuvunja mkataba wake na Yanga ikiwa ni siku chache zimepita tangu shauri lake litupiliwe mbali.
Feisal amefika Makao Makuu ya TFF akiwa ameongozana na Mwakilishi wake, Jasmin Razack wakiwa na barua mpya ya kuomba kuvunja mkataba wake na Yanga.
“Waandishi msikurupuke kwenye kusema Feisal kaonewa ama ameshindwa maneno mengi tuwe na uzalendo, ninaomba tuvute subra kwa mara ya kwanza leo, Feisal kaleta ombi lake naimani kama litashughulikiwa nina imani na TFF, chombo pekee kinachoweza kuvunja mkataba wa mchezaji ni TFF,” amesema Jasmin Razack.
Jasmin amewahi kusaidia Wachezaji mbalimbali kwenye migogoro ya kimkataba na klabu zao akiwemo Simon Msuva, Wilfred Bony aliyewahi kucheza Man City na Swansea City na Emmanuel Eboue aliyewahi kucheza Arsenal.