Feisal Salum 'Feitoto' arudi tena TFF na Wakili wa Msuva, aomba kuvunja mkataba na Yanga

Smart codetz

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2023
Posts
218
Reaction score
875
Feisal Salum “Feitoto” atinga tena TFF akiwa na aliyemsaidia Saimon Msuva kushinda kesi CAS. Mara hii amewasilisha barua ya maombi kwa TFF akitaka kuvunja mkataba wake na klabu yake ya YANGA



============
Mchezaji wa Klabu ya Yanga, Feisal Salum, Machi 6, 2023 amefika kwenye Ofisi za Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), Dar es Salaam kwa ajili ya kuwasilisha ombi kulitaka Shirikisho hilo kuuvunja mkataba wake na Yanga ikiwa ni siku chache zimepita tangu shauri lake litupiliwe mbali.

Feisal amefika Makao Makuu ya TFF akiwa ameongozana na Mwakilishi wake, Jasmin Razack wakiwa na barua mpya ya kuomba kuvunja mkataba wake na Yanga.

“Waandishi msikurupuke kwenye kusema Feisal kaonewa ama ameshindwa maneno mengi tuwe na uzalendo, ninaomba tuvute subra kwa mara ya kwanza leo, Feisal kaleta ombi lake naimani kama litashughulikiwa nina imani na TFF, chombo pekee kinachoweza kuvunja mkataba wa mchezaji ni TFF,” amesema Jasmin Razack.

Jasmin amewahi kusaidia Wachezaji mbalimbali kwenye migogoro ya kimkataba na klabu zao akiwemo Simon Msuva, Wilfred Bony aliyewahi kucheza Man City na Swansea City na Emmanuel Eboue aliyewahi kucheza Arsenal.
 
Kama anahitaji Kuvunja mkataba na Yanga ni ishu rahisi wala haitaji kwenda TFF. Timu yake ya ushauri ilitakiwa iende kuonana na uongozi wa Yanga Moja Kwa Moja. Maana hapo Sasa mnaongelea maslahi ya pande zote mbili.

TFF watakachomwambia arudi akaongee na uongozi wake kuhusu Kuvunja mkataba na ndicho Yanga walichokihitaji. Ila Sasa ni wazi Feisal hana watu sahihi wa kumuongoza au ushauri wa kitaalamu anaopewa haridhiki nao anataka vile yeye anavyo ona inafaa.
 
BREAKING NEWS

Feisal Salum “Feitoto” atinga tena TFF akiwa na aliyemsaidia Saimon Msuva kushinda kesi CAS. Mara hii amewasilisha barua ya maombi kwa TFF akitaka kuvunja mkataba wake na klabu yake ya YANGA
View attachment 2539157
Hata hawa mawakili hawana akili kabisa, bora angeenda kuongea na Engineer Hersi mwenyewe.....
 

Wanasheria wa Tanzania pumbavu kabisa, hawana cha kushauri mtu 😀😀😳😳😳😳 hii issue ni ya hiyari kwa Yanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…