Feisal Salum 'Feitoto' arudi tena TFF na Wakili wa Msuva, aomba kuvunja mkataba na Yanga

Feisal Salum 'Feitoto' arudi tena TFF na Wakili wa Msuva, aomba kuvunja mkataba na Yanga

Fei Kaonewa Nn?, Alikuwa Halipwi?,Alikuwa Hachezi?,Alilazimishwa Kusaini Huo Mkataba Wa Million 4?, Amezuiliwa Kuondoka Hapo Yanga? Au Wanachotaka Yanga Ni Yeye Kufuata Utaratibu Wa Namna Ya Kuondoka Hapo Yanga?
Aambiwe huo utaratibu aondoke zake. Huu utaratibu mbona ni siri kubwa hivi? Kama alikosea si anaambiwa alipokosea na ni nn cha kufanya? asahihishwe kwa kuambiwa ni nn afanye aondoke. Kila siku utaratibu, utaratibu mchezaji hataki kuwepo kikosini. Yanga imwambie wazi, ukitaka kuondoka fanya A,B,C vile ulivyofanya sio sawa kwa sababu A,B,C.
 
Sawaa ila kilichofuata ni nini? Pande zote mbili zililimaliza na maisha yakaendelea. Hilo ndilo post ile inauliza, kinachozuia pande hizi mbili kulimaliza suala lao ni nini?

Yanga hawawezi kuendelea milele kujificha kwenye kivuli cha "aje mezani tuongee". Mkataba umekiukwa, dogo hataki kuendelea kucheza, nini kinafuata? Je akitangaza kustaafu kucheza soka akavue pweza mtaendelea kumtumia mshahara wake?
Mkataba wa faisal na yanga bado ni halali na tff wameshatoa maelezo juu ya hilo sasa kama Faisal kama anataka kuvunja mkataba afike ofisi za Yanga tumtajie dau la kuvunja mkataba huko TFF alipoenda kaingia chaka ataambiwa aende Yanga kumalizana napo.
 
mbona Makambo na Bigirimana walivunjiwa kirahisi tu katikati ya msimu?
 
Aambiwe huo utaratibu aondoke zake. Huu utaratibu mbona ni siri kubwa hivi? Kama alikosea si anaambiwa alipokosea na ni nn cha kufanya? asahihishwe kwa kuambiwa ni nn afanye aondoke.
Utaratibu kesho aje ofisi za Yanga tumpe maelekezo kabla mawakili pori hawajamfilisi.
 
Muda wa kumuacha huyu kijana ndo sasa....zile hela wachukue..
Kwa ilivyofikia hawezi kurudi akawa na amani..
Sure. Nadhani Yanga wakubali kuvunja mkataba na kulipwa fidia ya uvunjaji huo. Naamini Feisal na wadau wake wana pesa ya kuwalipa Yanga
 
Utaratibu kesho aje ofisi za Yanga tumpe maelekezo kabla mawakili pori hawajamfilisi.
Utaratibu mpeni wazi mashabiki zenu wazifahamu. Siri za nn na mtu keshawashtaki? Hela haikutosha aliyoweka?
 
Muda wa kumuacha huyu kijana ndo sasa....zile hela wachukue..
Kwa ilivyofikia hawezi kurudi akawa na amani..
Yanga ni taasisi,taasisi yoyote inataka taratibu zifuatwe sio kuleta uhuni,taratibu zikifuatwa feisal mbona ataondoka tu Yanga tena kiulaini
 
Msuva alikua halipwi mshahara na kanuni zipo wazi.
Feisal ata aende CAS atarudishwa Kuja kumalizana na Yanga kwanza ndio apewe nafasi kwenda klabu nyingine.
CAS haijaundwa Ili kuvikamdamiza vilabu, na bahati Mbaya CAS uwa wanaomba ufafanuzi wa mgogoro uliopo na FA ya Nchi husika. Apo ndipo Feisal anakwenda ku unguzwa.
Watanzania ni debe tupu mkuu, kazi ya kupiga kelele bila ya sababu
Watu wanakazania kulinganisha kesi ya Msuva na Feisal bila hata ya kujua claim basis
Msuva alikua anawadai Raja signing fee, Fey amelipwa signing fee
Msuva alikua anadai malimbikizo ya mshahara, fey analipwa mshahara wake mpaka leo
Sasa mtu akaza shingo kisa wakili wa Msuva, ngoja tuone hatimae yake
 
Yanga ni taasisi,taasisi yoyote inataka taratibu zifuatwe sio kuleta uhuni,taratibu zikifuatwa feisal mbona ataondoka tu Yanga tena kiulaini
Taratibu zipi? Zile alizozifanya ni za kiuni, sahihi ni zipi? Anatakiwa kufanya nn?
 
Mkataba wa faisal na yanga bado ni halali na tff wameshatoa maelezo juu ya hilo sasa kama Faisal kama anataka kuvunja mkataba afike ofisi za Yanga tumtajie dau la kuvunja mkataba huko TFF alipoenda kaingia chaka ataambiwa aende Yanga kumalizana napo.
Sawaa atakuja kesho saa 3 asubuhi ofisi za GSM 🤣😂🤣
 
Back
Top Bottom