Feitoto agoma kurudi Uto, ataka review ya hukumu ya TFF

Asijipotezee muda, aende CAS, hapo TFF kumejaa wanasiasa tu, ukiona watu wanapata kigugumizi siku mbili kutoa maamuzi, wakati kila kitu kipo wazi kwenye mkataba, ujue hamna maana hapo...

Ni kijiwe cha wahuni tu.
Sio kwamba anapoteza muda ila Wanasheria wake ni Mbumbumbu mno, Huwezi kukata rufaa au kuomba review kwenye mamlaka iliyotoa uamuzi. Ilitakiwa aombe mwenendo wa shauri ili aende kukata rufaa kwenye ngazi inayofuata yaani CAS. Halafu hata sababu ambazo Wanasheria wake wanazitumia katika ku-justify review ni za kilimbukeni zaidi. Huwezi kusema mchezaji hapendi tena kuchezea timu fulani, wanatakiwa wajikite kwenye masuala yaliyovunjwa kwenye Mkataba kati ya Yanga na Feisal.
 
Mpaka muda huu ubao wa matokeo unasoma hivi;
Yanga 3 - Fei Toto+Azam fc+Dubai fc+mashabiki wa Dubai
Fc+wachambuzi uchwara 0!
 
Endeleeni kumponza .....
 
Yusufu Bareksa mtoto wa bilionea ndiye yupo nyuma ya Feisal ndio maana Feisal anapata Kiburi.
Mwishowake Feisal mpira utamshinda na ata ajiliwa kama Dereva katika Moja ya makampuni ya Azam hivi ndivyo maranyingi hutokea.
Tuone sasa hiyo jeuri yake ya pesa kama ina uwezo wa kushindana na Wananchi wa Tanzania.
 
Hivi kwann mnaendeshwa na mahaba hata sehemu zisizostahiki.

Yaani unakubali kuwa hakuvunja mkataba kihalali hivyo aadhibiwe lakini unasahau kuwa mkataba usiovunjwa kihalali Ni mkataba usiovunjwa.

Unakubali kabisa FEI anastahili kuadhibiwa ila unalazimisha kuwa mkataba umevunjwa. Sasa kama kavunja mkataba kwa hivyo vifungu vyako unavyotaka kwann unataka aadhibiwe?

We unajua mambo ya mikataba hivi kweli?

Umewahi kupanga nyumba? Kwahiyo mwenye nyumba anaweza kuamka asubuhi tu akakutolea vitu nje na Kisha kusema kavunja mkataba alafu serekali ya mtaa au ukienda mahalamani waseme ni kweli mwenye nyumba alikosea hakuvunja mkataba vizuri kwa hiyo anaadhibiwa kulipa fine ila wewe utajijua huko uliko kama vitu viko barabarani au chini ya mti haijalishi mradi ameshaadhibiwa kulipa fine

Hebu eleweni kitu kimoja aisee MKATABA USIOVUNJWA KIHALALI NI MKATABA USIOVUNJWA NA UNAENDELEA VILE VILE ULIVYOKUWA.

Mnamdanganya huyu mtoto, mtaharibu future yake. Nyie mko makwenu na makazini kwenu mnamdanganya huyu dogo wakati mpira ndio kazi yake
 
... hivi Yanga wamemkosea nini huyu kijana? Mbona alikuwa anawabeba sana; nini kimetokea ghafla wameshindwana?
Mwenye makosa ni huyo dogo. Akiwa ndani ya mkataba na klabu yake mpaka 2024, from nowhere anakubali kurubuniwa na matapeli, na hivyo kusitisha mkataba wake na klabu kinyume na kanuni/sheria za zilizowekwa na FIFA.

Kama alikuwa hana mahaba na Yanga, kwa nini alisaini mkataba wa kuichezea? Na kama aliona mshahara ni mdogo, kwa nini alikubali kusaini mkataba?

Na kama alikuwa anataka kuhamia timu nyingine, utaratibu unaotakiwa ni wa kuingiza hela kwenye klabu yako pasipo makubaliano, au timu husika ilitakiwa kukaa mezani na Yanga ili kumnunua?
 
Hoja ipi na ashaambiwa akiona hajatendewa haki aende CAS?
Je kama kuomba marejeo ndiyo sehemu ya hatua za kwenda CAS? Kamati inakumbushwa kujikita kwa hoja iliyokuwepo ambayo ni Je uvunjaji wa mkataba ulifuata taratibu ama la? Na kama alivunja mkataba bila taratibu kufuatwa basi aadhibiwe kwa kosa hilo.Kumlazimisha kurudi Yanga siyo sehemu ya hoja iliyopelekwa mbele ya Kamati.
 
Utopolo ni kikundi cha wachawi ndo kilicho sababisha mpaka sasa ngasa ni masikini baada ya kuharibu dili ambalo linge mpatia milion 300
 
Ingekuwa sheria na mikataba vinaendeshwa kwa maoni yako basi hii dunia isingekuwa sehemu Salama ya kuishi.

Rage alikuwa sahihi sana kuwaita mbumbumbu na kwenye hili amejitenga na mambumbumbu na amesema wazi Fei Toto hata aende CA's ni wasting of money hakuna anapoweza kushinda.

Nadhani Mambumbumbu mnamjuwa vizuri Rage kwenye sheria za mpira yuko vizuri kiasi gani, watu wenye akili huwa tunasikiliza maoni ya prominent figure kama Rage na siyo wanywa wanzuki waliomka na hangover ya smart.
 
Hizi taarifa za ndani sanaa🤣🤣🤣
 
... shukran kwa ufafanuzi. Changamoto nyingine za wachezaji wetu hawa ni shule na uelewa mdogo. Sina hakika kama alipokuwa anasaini huo mkataba alifahamu maana na atahri zake sembuse hata kuusoma na kuuelewa kabla ya kusaini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…