Feitoto agoma kurudi Uto, ataka review ya hukumu ya TFF

Pesa zilizo tokana na wizi wa pesa za uma.
 
Sasa wewe unaona hilo liko sawa?

Shauri lilopelekwa mahakamani na Yanga linaongelea kitu kingine lakini hukumu iliyokuja ina base kwenye kitu kingine ambacho hakihusiani na shauri liloletwa

Hiyo unaiona sawa?
 
Waliopeleka shitaka TFF ni Feisal au Yanga? Mbona mnajitoa ufahamu? Yaani Kamati imekubaliana na hoja ya mpeleka shitaka halafu mnataka ihukumu ambacho haijaombwa kwenye madai?
Kwani mpaka saizi TFF imehukumu ilicholalamikiwa?
 
Fei Toto hastahili kulipwa kiasi hicho cha pesa. Sioni mfano wowote duniani wa kuhalalisha hilo.
Yanga ya sasa bila Fei inawezekana. Yanga kumpa maslahi bora Fei iliwezekana.
 
Mkuu hata wewe jifikirie tu, Feisal katika ubora ule aliokuonesha uwanjani ambao ni zaidi ya hao wanaochukua 20+M, hivi kwa mtu mwenye busara unaweza ukasubiria uombwe kuongeza mshahara wakati unaona?


Halafu kwenye ishu ya mkataba wakumlaumu hapo ni aliyeandika mkataba wa Feisal

Aliyeandika mkataba ndiye aliyeweka kipengele kinachomruhusu Feisal kuvunja mkataba as long as atalipa 100M na 12M ya mshahara

Na ndio maana hata utetezi wa Yanga mahakamani ulikuwa unajikita kwenye neno "controversial" kuwa Feisali hakutafsiri vizuri hilo neno.
 
We jamaa ni PUNGUWANI.

Kwahiyo angeshuka kiwango mashahara angeshushwa?
 
Kilete hapa hicho kipengere tukione
 
Kuna vitu hua unatumia sio bure
 
Hivi nyie mbumbumbu mna akili kweli? Mnajiona mnaujua sana mkataba wa fei kuliko waliouandika? Kwa akili zenu nusu mnajua kwenye mkataba kuna kipengele kimoja tu basi, mmekomaa na kipengele cha cha kulipa pesa kama vile mmekaririshwa ngonjera? Mkataba ni vipengele vyote vilivyomo kwenye mkataba husika na sio mnavyowaza nyie ndani ya vichwa vyenu endeleeni kumjaza ujinga tuone ataishia wapi
 
Fei Toto hastahili kulipwa kiasi hicho cha pesa. Sioni mfano wowote duniani wa kuhalalisha hilo.
Yanga ya sasa bila Fei inawezekana. Yanga kumpa maslahi bora Fei iliwezekana.
Kwani huyo Fei Toto alishawahi kukulalamikia kulipwa ujira mdogo? Alipokuwa JKU alikuwa analipwa milioni ngapi?

Alishindwa nini kukaa na viongozi wake wa timu ili kuboresha maslahi ya mkataba wake? Na badala yake akachagua kutumia njia ya mkato, baada ya kurubuniwa na matapeli wa soka?
 
Unaifahamu mishahara ya wachezaji wenu wote wa simba? Mishahara ya wazawa inalingana na ile ya wageni? Yaani Kibu Dennis analipwa mshahara sawa na Clotus Chama, au Moses Phiri?

Unafiki ni mbaya sana. Mnapoteza muda mwingi kufuatilia matatizo ya wengine, wakati ya kwenu yanawashinda.
 

Ushajiuliza viongozi wa Yanga waliposema walikuwa wanazungumza na mwakilishi wa fei kuhusu maslahi yake kama waliombwa na fei au walijiamulia?

Kwann usiulize viongozi sababu za kutoboresha maslahi ya Fei ndani ya muda yakalingana na mchango wake? Na kwann unadhani Fei hakuomba aboreshewe maslahi kabla ya kufanya hili alilofanya?

Au ndo zile roho zetu za kitanzania za HUYU WETU, HANA SHIDA HUYU, VUTENI VUTENI KWANZA TUSAVE MAPATO KWANZA UKIMPA HELA NYINGI HUYU ATAISHIA KUFANYA STAREHE halafu akitokea mtu anayeitambua thamani yake ndo watu wanajifanya walikuwa kwenye mchakato.

Yale yale ya kutokumchangia mgonjwa ila akifa michango kede kede.
 
Kwahio unatakaje mbona haueleweki
 
Afate utaratibu
Mm ningekuwa shabiki wa Yanga nisingekuwa upande wa viongozi na kichaka chao cha kufuata taratibu. Ningewahoji kwa kutokuthamini mchango wa kijana mzawa.

Sawa Fei alisain mkataba kabla hatujakiona hichi kiwango ndo maana mkataba ulikuwa wa thamani ndogo, ila baada ya kukiona kiwango kwann hatukuwa wa kwanza kumshawishi na mkataba wenye maslahi bora mpaka waje wengine kutoka nje?

Kuna harufu ya viongozi fulani fulani hapo kumnyonya Fei. Na tunajua akili za baadhi ya wabongo wakiwa wameshika mpini. Unaweza kuta Fei alishaomba sana tu wamwangalie ila zile roho fulani hivi zikasababisha wasijali na kuchukua hatua kwa wakati na sasa hivi watavaa ukondoo chini ya kivuli cha taratibu hazikufuatwa.

WANAYANGA WATAFUTE CLIP ZA FEI AKIIPIGANIA YANGA HALAFU WAJIULIZE, YULE ANAFANANA NA MCHEZAJI ALIYEICHUKIA YANGA NA KUTAKA ATOROKE ISIPATE CHOCHOTE? SIKU AKIWA ANASTAAFU ANAWEZA ONGEA YALIYOMKUTA.
KWA SASA ATATULIA KWANI HAKUNA MCHEZAJI MKUBWA KULIKO CLUB NA NI HATARI KUZUNGUMZIA CLUB ULIYOTOKA VIBAYA WAKATI BADO UNAHITAJI CLUB NYINGINE IKUSAJILI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…