Nilikuwa juzi kati hapa naangalia mkeka wa mshahara wa klabu ya Man City; mchezaji kama Julian Alvarez aliyeisaidia timu yake ya Argentina kuchukua ubingwa wa kombe la Dunia 2022, anapokea paundi 50,000/= tu kwa wiki! Huku Kelvin De Bruyne akiwa ndiye kinara kwa kupokea zaidi ya paundi laki 3 na ushee!
Umeona analalamika? Hapana! Kwa sababu amesaini mwenyewe mkataba wa kujiunga na klabu hiyo kwa malipo hayo. Muda wake na yeye wa kupandishiwa mshahara ukifika, atafanyiwa hivyo.
Hivyo mnatakiwa muwashauri na akina Fei Toto kuwa wavumikivu, na pia kufuata utaratibu kama hawaridhiki na mishahara wanayolipwa. Siyo mnakubali tu akina Yusuph Bakhressa kutumia hela zao kutuharibia mpira wetu kwa kuwarubuni wachezaji kuvunja mikataba kienyeji, kwa kisingizio cha malipo kiduchu.
Au unataka uniambie na yeye kwenye timu yake ya Azam, anawalipa wachezaji wake wote (na hasa wazawa) mshahara sawa wa milioni 17 kwa mwezi? Nongwa iko wapi kwa Fei Toto kulipwa milioni 4 alizo ridhia mwenyewe kwenye mkataba?