Feitoto ana gundu kuachwa tena Stars?

Feitoto ana gundu kuachwa tena Stars?

Jana kocha wa Taifa Stars, Adel Amrouche amemuacha tena kiungo wa Azam FC, Feisal Salum 'Feitoto' na Jonas Mkude kwenye kikosi kitakachocheza dhidi ya Sudan.

Hii inakuwa mara ya pili mfululizo kwa Feitoto kuachwa na Amrouche akitangulia kukosa mechi dhidi ya Niger na Algeria, wakati Taifa Stars ikisaka tiketi ya kushiriki fainali za Mataifa ya Afrika, nchini Ivory Coast.

Mara ya mwisho Amrouche kumuita Fei toto ni pale alipochaguliwa kuingia katika kikosi hicho katika mechi mbili dhidi ya Uganda, mchezo ulichezwa katika Uwanja wa Mkapa, Machi 28, baada ya ule uliofanyika Morocco.

Taifa Stars imeshaingia kambini ikijiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Sudan utakaofanyika nchini Saudi Arabia na kikosi hicho kitaondoka nchini leo kwenda nchini humo.

Kikosi hicho kitaondoka na wachezaji 26 wanaocheza ndani na nje ya nchi, wakiwemo makipa Beno Kakolanya, Metacha Mnata na Ally Salum.

Kocha wa zamani wa Yanga, Charles Mkwasa alisema kilichokea wakati wa mechi za mwisho za kufuzu kwa Afcon 2023 ndicho kilichopo kwa sasa na kocha (Amrouche) anatakiwa kuheshimiwa katika uamuzi wake.

"Mwanzo ilionekana kama hakufanya sawa, lakini nini kilitokea? Malengo yake yalitimia. Hata sasa tunaweza kumlaumu lakini hatutakuwa tunatenda haki, kwani yeye ndiye kocha na anajua nini anafanya," alisema kocha huyo wa zamani wa Ruvu Shooting.

Mabeki kwenye kikosi hicho ni Israel Patrick Mwenda(Simba), Abdulrazak Mohamed Hamza (Supersport United), Nickson Kibabage, Ibrahim Abdullah 'Bacca', Bakari Mwamnyeto, Dickson Job (Yanga) na Abdulmalik Adam (Mafunzo). Viungo ni Sospeter Bajana (Azam FC), Kibu Denis, Mzamiru Yassin (wote Simba), Baraka Majogoro (Chippa United), Mudathiri Yahya (Yanga), Abdi Banda, Abdulmalik Adam, Novatus Dismas (FC Shaktar) Wakati washambuliaji ni George Mpole (FC Lupopo), Said Khamis (Jedinstvo Ub), Nassor Saadun (Ihefu), Morice Michael, Ben Anthony, Saimon Msuva (JS Kabylie) na Mbwana Samatta (PAOK).
Binadamu huvuna alichopanda
 
Wazungu hawanaga ubabaishaji..hawa watoto, fey na mkude ni viburi na wasaliti. Hivyo huwezi kuambatana na mtu kiburi na mwenye usaliti.
Kama mfanyakazi tena wa chini kabisa, anathubutu kusema Rais akiondoka mimi nitarudi kufanya kazi, unategemea mtu wa ainahii hatakama ni mtoto anaakili sawasawa kweli?
Acha aendelee kula askilim na kulipwa huo mshala wake mkubwa aliokua anautaka.
 
Simba na yanga ni madrid na Barcelona za Tanzania,........ Tafakari!!!!! mengine utajiongeza sio lazima kila kitu ufundishwe kwenye hii dunia.
Na nyongeza ya hapo, mpira wa Tanzania ni Simba na Yanga. Ukiwatunishia misuli ujue humtunishii Hersi au Try again
 
Mbavu za Simba ni uchochoro for now, Huwa hawajitumi Taifa Stars, mjadala wao umefungwa!

Feitoto kurudi Stars ni majaaliwa, ishu ni namna anacheza Azam. Akiwa Yanga mfumo wa uchezaji wa timu ya Yanga ulimpa nafasi ya kuonesha kipaji chake, hilo halipo Azam! But I believe one day atarudi Stars ila sio Leo mpaka aombe msamaha wazee, mashabiki na viongozi wa Yanga!
Anasemaga Oscar elewa neno "Wazee"
 
feitoto alikuwa overrated, na alijiamini kwamba yeye ndio yeye bila yeye hakuna mafanikio, kumbe ni mla urojo tu. aende akatetewe na sa100 tena, atoe maelekezo wamuweke kwenye kikosi cha taifastars. mpira wake ndio umeishia hapo. anajua kupiga mashuti tu hana hana uwezo wa kutosha.
 
Jana kocha wa Taifa Stars, Adel Amrouche amemuacha tena kiungo wa Azam FC, Feisal Salum 'Feitoto' na Jonas Mkude kwenye kikosi kitakachocheza dhidi ya Sudan.

Hii inakuwa mara ya pili mfululizo kwa Feitoto kuachwa na Amrouche akitangulia kukosa mechi dhidi ya Niger na Algeria, wakati Taifa Stars ikisaka tiketi ya kushiriki fainali za Mataifa ya Afrika, nchini Ivory Coast.

Mara ya mwisho Amrouche kumuita Fei toto ni pale alipochaguliwa kuingia katika kikosi hicho katika mechi mbili dhidi ya Uganda, mchezo ulichezwa katika Uwanja wa Mkapa, Machi 28, baada ya ule uliofanyika Morocco.

Taifa Stars imeshaingia kambini ikijiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Sudan utakaofanyika nchini Saudi Arabia na kikosi hicho kitaondoka nchini leo kwenda nchini humo.

Kikosi hicho kitaondoka na wachezaji 26 wanaocheza ndani na nje ya nchi, wakiwemo makipa Beno Kakolanya, Metacha Mnata na Ally Salum.

Kocha wa zamani wa Yanga, Charles Mkwasa alisema kilichokea wakati wa mechi za mwisho za kufuzu kwa Afcon 2023 ndicho kilichopo kwa sasa na kocha (Amrouche) anatakiwa kuheshimiwa katika uamuzi wake.

"Mwanzo ilionekana kama hakufanya sawa, lakini nini kilitokea? Malengo yake yalitimia. Hata sasa tunaweza kumlaumu lakini hatutakuwa tunatenda haki, kwani yeye ndiye kocha na anajua nini anafanya," alisema kocha huyo wa zamani wa Ruvu Shooting.

Mabeki kwenye kikosi hicho ni Israel Patrick Mwenda(Simba), Abdulrazak Mohamed Hamza (Supersport United), Nickson Kibabage, Ibrahim Abdullah 'Bacca', Bakari Mwamnyeto, Dickson Job (Yanga) na Abdulmalik Adam (Mafunzo). Viungo ni Sospeter Bajana (Azam FC), Kibu Denis, Mzamiru Yassin (wote Simba), Baraka Majogoro (Chippa United), Mudathiri Yahya (Yanga), Abdi Banda, Abdulmalik Adam, Novatus Dismas (FC Shaktar) Wakati washambuliaji ni George Mpole (FC Lupopo), Said Khamis (Jedinstvo Ub), Nassor Saadun (Ihefu), Morice Michael, Ben Anthony, Saimon Msuva (JS Kabylie) na Mbwana Samatta (PAOK).
Aitwe kwa mpira upi?
 
Kwa watu walioangalia mechi za Azam hawatashangaa hata kidogo. Ameonesha uwezo mdogo sana, na nadhani pia anampa wakati mgumu sana kocha wa Azam. Hata huko nahisi kocha atakuwa ameambiwa ni lazima acheze. Apambane kuinua kiwango tu.
Well said.
 
Mbavu za Simba ni uchochoro for now, Huwa hawajitumi Taifa Stars, mjadala wao umefungwa!

Feitoto kurudi Stars ni majaaliwa, ishu ni namna anacheza Azam. Akiwa Yanga mfumo wa uchezaji wa timu ya Yanga ulimpa nafasi ya kuonesha kipaji chake, hilo halipo Azam! But I believe one day atarudi Stars ila sio Leo mpaka aombe msamaha wazee, mashabiki na viongozi wa Yanga!
Yule dogo alikuwa na wivu baada ya kuja Ki Azizi huku akilipwa mshahara mkubwa kuliko yeye, wakati vilabu vyote vya mpira duniani mishara ya wachezaji haifanani, unaweza ukawa na kiwango Bora na mwenzio akawa na kiwango duni lkn bado akakuzidi mshahara kutokana na mkataba mliokubaliana.
 
Fei alisha shinda vita yake, Yeye alihitaji maokoto zaidi kuliko kipaji chake.
Katika moja ya Mazungumzo ya Mayele anasema wakati wanakwenda kucheza na club African Feisal alimwambia anaondoka Yanga, Yeye akamshauri subiri msimu uishe ndio asepe.
Feisal angekua na subira kidogo kwasasa ungeweza kuta Yupo kwa waarabu na mshahara wa zaidi ya milioni 70.

Kwakua Feisal alikua kwenye kiwango cha juu siku hadi siku, Kitendo cha kuanzisha mgogoro na klabu yake kwa maokoto ya Azam ndio gharama anazolipia kwasasa.

Maokoto anapata ila uzito umeongezeka na mpaka sasa bado hajafikia kile kiwango chake.

Anacho takiwa ni kuongeza juhudi kwenye mazoezi ili afike pale alipo ishia na kusonga mbele
.
Yeye mwenyewe amekiri mazingira ya Azam ni mazuri, Apambane kurudisha uwezo alio wahi kuwa nao.
Yanga alikua anashindia ugali na sukari, Azam anashindia Ice Cream, soudage, chapati na mapochopocho mengine, kwanini asiongezeke uzito?
 
Back
Top Bottom