Fei alisha shinda vita yake, Yeye alihitaji maokoto zaidi kuliko kipaji chake.
Katika moja ya Mazungumzo ya Mayele anasema wakati wanakwenda kucheza na club African Feisal alimwambia anaondoka Yanga, Yeye akamshauri subiri msimu uishe ndio asepe.
Feisal angekua na subira kidogo kwasasa ungeweza kuta Yupo kwa waarabu na mshahara wa zaidi ya milioni 70.
Kwakua Feisal alikua kwenye kiwango cha juu siku hadi siku, Kitendo cha kuanzisha mgogoro na klabu yake kwa maokoto ya Azam ndio gharama anazolipia kwasasa.
Maokoto anapata ila uzito umeongezeka na mpaka sasa bado hajafikia kile kiwango chake.
Anacho takiwa ni kuongeza juhudi kwenye mazoezi ili afike pale alipo ishia na kusonga mbele
.
Yeye mwenyewe amekiri mazingira ya Azam ni mazuri, Apambane kurudisha uwezo alio wahi kuwa nao.