Feitoto yupo sawa kisheria

Feitoto yupo sawa kisheria

Decree Holder

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2015
Posts
2,559
Reaction score
3,745
Nimesikia mwanasheria na uongozi wa Yanga wanasema Feitoto hajafuata utaratibu uliopo kwenye kanuni za FIFA za kuvunja mkataba ambapo mchezaji ili avunje mkataba lazima kuwe na just cause (reasonable cause).

Kitu ambacho tunatakiwa tujue ni kwamba kanuni za FIFA siyo alfa na Omega bali zinatoa minimum standards tu, nadhani wanasheria wenzangu mtakubaliana na mimi, hii ipo hata kwenye sheria za kawaida za kazi hazielezi kila kitu exactly bali zinatoa minimum standards (viwango vya chini) ambavyo havitakiwi kuvukwa.

Kuweka kigezo cha ili upande mmoja uvunje mkataba lazima kuwe na just cause lengo ni kulinda mikataba ya wachezaji ili isivunjwe hovyo, kwakuwa hiyo ni minimum requirement haizuii timu na mchezaji kuboresha na Kuja na terms bora zaidi kwa ajili ya kulinda zaidi mikataba ya wachezaji.

Na katika kufanya hivyo ndiyo maana Yanga na Feitoto katika mkataba wao wakaweka masharti iwapo mchezaji atataka kuvunja mkataba bila sababu ya msingi arudishe signing fees na mishahara ya miezi 3.

Mawakili wa Yanga hawakuweka kipengele hiki kwa bahati mbaya bali lengo lilikuwa ni kuset higher standards than those under FIFA rules ili kulinda maslahi yao kama timu kwa kuzuia mikataba kuvunjwa hovyo. Pia ilikuwa ni higher standard kumpa freedom of movement mchezaji aweze kuvunja mkataba bila kuwa na just cause ila tu kwa kulipa amount fulani ya pesa, favorable terms kwa weak party au zinazoraise standard zinaruhusiwa kisheria

Kwa mujibu wa kanuni za FIFA mchezaji anapovunja mkataba kukiwa na just cause hatakiwi kulipa fidia au pesa ya aina yoyote ile, hivyo kwa tafsiri ya haraka haraka hakukuwa na haja ya kumtaka mchezaji alipe fidia pale anapovunja mkataba for just cause hivyo ni wazi kipengele cha kwenye mkataba wa Yanga na Feitoto kumtaka alipe milioni 112, kililenga kutumika pale anapokuwa hana sababu ya msingi.

Sasa kama mchezaji amefuata mkataba unavyotaka haiwezekani akawa subjected tena kwenye minimum standards za FIFA wakati ametekeleza maximum standards zilizomo ndani ya mkataba.

Mwisho nimeona mwanasheria wa Yanga anasema bado Feitoto ni mchezaji wa Yanga kwa kuwa hajafuata utaratibu, huo ni upotoshaji.

Kwa uelewa wangu wa sheria termination of contract/kuvunja mkataba ni kufanya mkataba ufike mwisho, hata kama itagundulika kwamba Feitoto hajafuata taratibu katika kuvunja mkataba bado haimaanishi mkataba haujavunjika la hasha.

Itakuwa ni unlawful termination ambayo kwa mujibu wa ibara ya 17 ya kanuni za FIFA mchezaji anaweza kupigwa sanctions na Yanga wanaweza kulipwa fidia lakini kanuni za FIFA hazitoi remedy wa kumlazimisha mchezaji aliyevunja mkataba kimakosa kurudi kuichezea timu yake.

Hivyo siyo Sawa kwa mwanasheria wa Yanga kusema Feitoto bado ni mchezaji wa Yanga whether alifuata utaratibu au la katika kuvunja mkataba.

Ndimi Wakili Zawadi B Lupelo
 
Nmecheka eti katika mkataba wao hakuna kipengele cha kuvunja [emoji23][emoji23][emoji23] yan mkataba usiwe na kipengele cha kuvunja [emoji23][emoji23][emoji23] hiyo 112m ni ya nn sasa? kwahiyo fei kaamka tu kaenda bank kudeposit 112m tu kwanini isiwe 23m 75m au 98m. kwa sababu kuna kipengele cha kuvunja na sharti ni signing fee irudishwe na mshahara wa miezi 3.
Nadhani yanga walidhani kibongo bongo hakuna mchezaji ataweza kutoa hiyo 100m kulipa kuvunja mkataba. Waamke mambo amebadilika. Halafu waache kuwaadaa mashabiki. Wamtakie kila la kheri maisha mzunguko iko siku atarejea.
 
Nimesikia mwanasheria na uongozi wa Yanga wanasema Feitoto hajafuata utaratibu uliopo kwenye kanuni za FIFA za kuvunja mkataba ambapo mchezaji ili avunje mkataba lazima kuwe na just cause (reasonable cause).

Kitu ambacho tunatakiwa tujue ni kwamba kanuni za FIFA siyo alfa na Omega bali zinatoa minimum standards tu, nadhani wanasheria wenzangu mtakubaliana na mimi, hii ipo hata kwenye sheria za kawaida za kazi hazielezi kila kitu exactly bali zinatoa minimum standards (viwango vya chini) ambavyo havitakiwi kuvukwa.

Kuweka kigezo cha ili upande mmoja uvunje mkataba lazima kuwe na just cause lengo ni kulinda mikataba ya wachezaji ili isivunjwe hovyo, kwakuwa hiyo ni minimum requirement haizuii timu na mchezaji kuboresha na Kuja na terms bora zaidi kwa ajili ya kulinda zaidi mikataba ya wachezaji.

Na katika kufanya hivyo ndiyo maana Yanga na Feitoto katika mkataba wao wakaweka masharti iwapo mchezaji atataka kuvunja mkataba bila sababu ya msingi arudishe signing fees na mishahara ya miezi 3.

Mawakili wa Yanga hawakuweka kipengele hiki kwa bahati mbaya bali lengo lilikuwa ni kuset higher standards than those under FIFA rules ili kulinda maslahi yao kama timu kwa kuzuia mikataba kuvunjwa hovyo.

Kwa mujibu wa kanuni za FIFA mchezaji anapovunja mkataba kukiwa na just cause hatakiwi kulipa fidia au pesa ya aina yoyote ile, hivyo kwa tafsiri ya haraka haraka hakukuwa na haja ya kumtaka mchezaji alipe fidia pale anapovunja mkataba for just cause hivyo ni wazi kipengele cha kwenye mkataba wa Yanga na Feitoto kumtaka alipe milioni 112, kililenga kutumika pale anapokuwa hana sababu ya msingi.

Sasa kama mchezaji amefuata mkataba unavyotaka haiwezekani akawa subjected tena kwenye minimum standards za FIFA wakati ametekeleza maximum standards zilizomo ndani ya mkataba.

Mwisho nimeona mwanasheria wa Yanga anasema bado Feitoto ni mchezaji wa Yanga kwa kuwa hajafuata utaratibu, huo ni upotoshaji.

Kwa uelewa wangu wa sheria termination of contract/kuvunja mkataba ni kufanya mkataba ufike mwisho, hata kama itagundulika kwamba Feitoto hajafuata taratibu katika kuvunja mkataba bado haimaanishi mkataba haujavunjika la hasha.

Itakuwa ni unlawful termination ambayo kwa mujibu wa ibara ya 17 ya kanuni za FIFA mchezaji anaweza kupigwa sanctions na Yanga wanaweza kulipwa fidia lakini kanuni za FIFA hazitoi remedy wa kumlazimisha mchezaji aliyevunja mkataba kimakosa kurudi kuichezea timu yake.

Hivyo siyo Sawa kwa mwanasheria wa Yanga kusema Feitoto bado ni mchezaji wa Yanga whether alifuata utaratibu au la katika kuvunja mkataba.

Ndimi Wakili Zawadi B Lupelo
Kwahiyo ndugu mwanasheria mkataba unapovunjwa inakuaje? Lazima kuwe na mazungumzo au najiamulia tu kuwarudishia pesa yao kama Mkataba unavosema ?
 
Nmecheka eti katika mkataba wao hakuna kipengele cha kuvunja [emoji23][emoji23][emoji23] yan mkataba usiwe na kipengele cha kuvunja [emoji23][emoji23][emoji23] hiyo 112m ni ya nn sasa? kwahiyo fei kaamka tu kaenda bank kudeposit 112m tu kwanini isiwe 23m 75m au 98m. kwa sababu kuna kipengele cha kuvunja na sharti ni signing fee irudishwe na mshahara wa miezi 3.
Nadhani yanga walidhani kibongo bongo hakuna mchezaji ataweza kutoa hiyo 100m kulipa kuvunja mkataba. Waamke mambo amebadilika. Halafu waache kuwaadaa mashabiki. Wamtakie kila la kheri maisha mzunguko iko siku atarejea.
Imekula kwao
 
Kwahiyo ndugu mwanasheria mkataba unapovunjwa inakuaje? Lazima kuwe na mazungumzo au najiamulia tu kuwarudishia pesa yao kama Mkataba unavosema ?
Mwanasheria ameeleza vizuri hapo, kwa kuwa bado hujaelewa tukupe mfano mwepesi, Halaand amechukuliwa na City kwa kutumia sheria hiyo hiyo ya Release clause, mkifanikiwa kulipa Release clause hamuhitaji maongezi yoyote ya ziada na team ambayo mchezaji alikuwa anacheza.

Yanga wanune wazile ile Fei toto ndio ameshaondoka kwa pesa ndogo tu sababu ya ubahili wao.
 
Yanga wameshawaona mashabiki wao Kama kuku
 
Kwahiyo ndugu mwanasheria mkataba unapovunjwa inakuaje? Lazima kuwe na mazungumzo au najiamulia tu kuwarudishia pesa yao kama Mkataba unavosema ?
Mazungumzo ya nini kama alishawapa notice before kuvunja mkataba Yanga ndio ilibidi imfuate Feisal kuomba mazungumzo. Hadi amefikia kuvunja mkataba hajakurupuka kuna watu behind walisoma kile kipengele cha mkataba na wakajiridhisha yuko sahihi kufanya kilichofanyika.
 
Ni sawa nakusema hivi;

Mkataba unaweza kuvunjwa endapo kukiwa na moja kati ya haya!
1. Mpagaji hatakuwa amelipa kodi yake
2. Mpagaji asipoishi kwenye nyumba hiyo na kuifanyia usafi kwa mwaka mmoja
3. Endapo mwenye nyumba ataamua kubadili matumizi ya nyumba na kurudisha kodi ya mpangaji, pamoja na malipo ya usumbufu ya miezi mitatu ya ziada!

Done....................
Halafu mkataba wa namna hii ikitokea kipengele namba tatu kikazingatiwa! UPINGE kwa kusema cha kwanza hakijafuatwa hivyo ni batili, mwanasheria wa hovyo tu ambaye anapenda aonekane naye kafanya kazi kama ataamua kuleta ubishani!

WALITAKIWA WAMFUKUZE KAZI MWANASHERIA WA YANGA kwa umbumbumbu wa sheria! Waoneshe na vyeti vyake vinaweza kuwa na shida
 
Binafsi sioni ajabu kwa Fei kutaka kuondoka yanga kwasababu ndio maisha ya mpira ma wachezaji Duniani kote hutoka timu moja kwenda nyingine!!.
Kinachonishangaza hapa ni namna fei alivyoamua kuondoka yanga na namna ambavyo Azam na fei wameamu kufanya Mambo locally/kienyeji kiasi hiki!!, Fei kisheria mkataba wake hawezi kuuvunja pekee yake pasina malidhiano ya pande mbili. Lakini pia hata Kama mkataba wake unamruhusu afanye hivyo na yanga wakawa hawamruhusu njia sahihi ilikuwa sio hiyo anayoitumia!!, Kuna vyombo mahususi vya kushughulikia Mambo nyeti na haki za wachezaji je alizishirkisha ili kupata haki yake??.
Yanga na timu nyingine za Tz iwe fundisho kwenu kuheshimu wachezaji wazawa kwa maslahi ya mpira wetu, haiwwzekana mtu km Fei azidiwe mshahara na,
1.Makambo 10m
2.Gael 6m,
3.morrison 23m
Hii inatia kinyaa mchezaji anayejitoa kwa damu na jasho timu kupata MATOKEO kuzidiwa mshahara na watu wasio na mchango kwenye timu.
Binafsi ningekuwa na uwezo ningemuacha fei aende anakoona Kuna maslahi kwake.

Niwatakie Noel njema!
 
Ni sawa nakusema hivi;

Mkataba unaweza kuvunjwa endapo kukiwa na moja kati ya haya!
1. Mpagaji hatakuwa amelipa kodi yake
2. Mpagaji asipoishi kwenye nyumba hiyo na kuifanyia usafi kwa mwaka mmoja
3. Endapo mwenye nyumba ataamua kubadili matumizi ya nyumba na kurudisha kodi ya mpangaji, pamoja na malipo ya usumbufu ya miezi mitatu ya ziada!

Done....................
Halafu mkataba wa namna hii ikitokea kipengele namba tatu kikazingatiwa! UPINGE kwa kusema cha kwanza hakijafuatwa hivyo ni batili, mwanasheria wa hovyo tu ambaye anapenda aonekane naye kafanya kazi kama ataamua kuleta ubishani!

WALITAKIWA WAMFUKUZE KAZI MWANASHERIA WA YANGA kwa umbumbumbu wa sheria! Waoneshe na vyeti vyake vinaweza kuwa na shida
#3 yahusika. Eti tukae tukubaliane, tukubaliane nini wakati tukishakubaliana wakati tunasaini mkataba.
 
Mfano mzuri ni huku maofisini. Kuna kipengele cha mtu kuacha kazi kwa saa 24. Unarudisha mshahara wa mwezi unasepa. Huwezi kusema eti tukae mezani, tukae mezani wakati mimi nimevunja kwa mujibu wa mkataba . Tukae mezani kivipi wewe fala nini
Huo utaratibu kwenye ishu za Ulinzi au serikalini, ila kwa sehemu zinazojielewa lazima utoe notice si chini ya Mwezi.

Unaonekana ww hujaajiriwa.
 
We nae ni choko kweli haswa!! Niliwahi kukuuliza hii beji ya platinum uliipata kwa kutoa hoja za hivi au ulihongwa??.
Duniani kote watu siwanguvunja mkataba kma ndio rahisi hivi??, Kabla ya yeye kuvunja mkataba amezihusishaje taasisi za kimpira??, Acheni utahira na mihemko ya nyege mshindo!!
Dejan alipotangaza kuvunja mkataba kienyeji hukuona ngada fc mmekana huo utaratibu?.
Kama beji ya platinum member inatolewa kwa hoja Basi wewe hii beji umehongwq maana mi zero kabisa😅🙌🏃
 
#3 yahusika. Eti tukae tukubaliane, tukubaliane nini wakati tukishakubaliana wakati tunasaini mkataba.
Yes! Mkataba ndo makubaliano! Kwani kwenye kuuvunja huwa hakunaga nafas hiyo zaidi ya kuangalia maslahi yamefuata
 
Huo utaratibu kwenye ishu za Ulinzi au serikalini, ila kwa sehemu zinazojielewa lazima utoe notice si chini ya Mwezi.

Unaonekana ww hujaajiriwa.
Sio hajaariwa bali ana uwezo mdogo wa tafakuri.
 
Kwahiyo ndugu mwanasheria mkataba unapovunjwa inakuaje? Lazima kuwe na mazungumzo au najiamulia tu kuwarudishia pesa yao kama Mkataba unavosema ?
Kulipa hela ndio condition, hakuna sehemu yanapotajwa mazungumzo
 
Nadhani yanga walidhani kibongo bongo hakuna mchezaji ataweza kutoa hiyo 100m kulipa kuvunja mkataba. Waamke mambo amebadilika. Halafu waache kuwaadaa mashabiki. Wamtakie kila la kheri maisha mzunguko iko siku atarejea.
Hawaamini bado wanachoshuhudia.
 
Back
Top Bottom