Binafsi sioni ajabu kwa Fei kutaka kuondoka yanga kwasababu ndio maisha ya mpira ma wachezaji Duniani kote hutoka timu moja kwenda nyingine!!.
Kinachonishangaza hapa ni namna fei alivyoamua kuondoka yanga na namna ambavyo Azam na fei wameamu kufanya Mambo locally/kienyeji kiasi hiki!!, Fei kisheria mkataba wake hawezi kuuvunja pekee yake pasina malidhiano ya pande mbili. Lakini pia hata Kama mkataba wake unamruhusu afanye hivyo na yanga wakawa hawamruhusu njia sahihi ilikuwa sio hiyo anayoitumia!!, Kuna vyombo mahususi vya kushughulikia Mambo nyeti na haki za wachezaji je alizishirkisha ili kupata haki yake??.
Yanga na timu nyingine za Tz iwe fundisho kwenu kuheshimu wachezaji wazawa kwa maslahi ya mpira wetu, haiwwzekana mtu km Fei azidiwe mshahara na,
1.Makambo 10m
2.Gael 6m,
3.morrison 23m
Hii inatia kinyaa mchezaji anayejitoa kwa damu na jasho timu kupata MATOKEO kuzidiwa mshahara na watu wasio na mchango kwenye timu.
Binafsi ningekuwa na uwezo ningemuacha fei aende anakoona Kuna maslahi kwake.
Niwatakie Noel njema!