Feitoto yupo sawa kisheria

Hata ishu ya Thomas partey kwenda Arsenal,
 
haya ndo maelezo pekee niliyokuwa nayahitaji kuyasikia.

kwa maelezo ya mkataba wao unasema arudishe kiasi cha million 100 na mshahara wa miezi mitatu kama atataka kuvunja mkataba bila just cause. Sasa amevunja huo mkataba kwa kufuata term hiyo shida inakuja wapi?

Wengine wanatumia hisia kwa kusema et wakae chini waongee na yanga, kuhusu nini?ili iweje? Kwa sababu hajavunja kanuni yoyote ya kimkataba amefanya kama mkataba ulivyotaka.
 
Tukubali tu fei amevunja mkataba na amefuata taratibu za kuvunja,mkataba wowote una masharti jinsi ya kuuvunja kwa both parties....hakuna mkataba ambao hauna terms za kuterminate....Fei ameangalia akaona anaweza kuvunja na ndio maana akaenda kudeposit mzigo 112m
 
wameshamtakia kila la kheri, furahini na roho zenu.
 
TAARIFA KWA UMMA

KLABU ya Yanga inapenda kuujulisha umma na Wanachama wa Yanga kuhusiana na taarifa za mchezaji wetu Feisal Salum Abdallah zinazoenea katika mitandao ya kijamii.

Klabu inathibitisha kupokea barua kutoka kwa mchezaji tarehe 23 Disemba 2022 inayoeleza kuvunja Mkataba wake baina yake na Klabu.

Klabu ya Yanga imemuandikia na kumjibu Feisal na miongoni mwa majibu ni kama ifuatavyo;
1.Hakuna misingi ya kikanuni wala kisheria kulingana na mkataba wake ambazo zinampa haki mchezaji kusitisha mkataba wake na Klabu kwa mujibu wa makubaliano ya mkataba wa sasa
2.Kanuni na Taratibu za FIFA ziko wazi na zimeelezea taratibu zote juu ya Jambo la aina hii.
3.Kwamba, Mkataba baina ya mchezaji na Klabu hauwezi kuvunjwa na upande mmoja tu bila kujadiliana na upande wa pili wakati msimu wa ligi ukiwa unaendelea.
4.Kwamba, kwa mazingira hayo, barua ya mchezaji ina dhana potofu na haina misingi ya kisheria ya kuvunja mkataba baina ya klabu na mchezaji
5.Na kwa mantiki hiyo, tumemuagiza Feisal, azingatie matakwa ya mkataba wake kama ilivyoelezwa katika mkataba huo.
6.Klabu pia imemkumbusha Feisal, mkataba wake wa sasa ni halali hadi ifikapo Tarehe 30 Mei 2024

Pamoja na hayo, tunapenda kuujulisha umma kuwa, kwa kuthamini kiwango na mchango wa Faisal kwa klabu yetu, tayari tulishaanza mazunguzo baina ya klabu ya Yanga na wawakilishi wa Feisal wakiongozwa na mama mzazi wa mchezaji ili kuboresha maslahi yake na kuongeza muda wa mkataba wake wa sasa ambao unaishia Mei 2024.

Hata hivo, Klabu haijapokea majibu mbadala wa mapendekezo ya maboresho haya kutoka upande wa Feisal na wawakilishi wake na badala yake tumepokea barua inayoelezea kuvunja mkataba kutoka upande wa Feisal ambayo ni Kinyume na makubaliano ya mkataba wake wa sasa.

Klabu tayari imesharejesha fedha kiasi cha TZS 112,000,000 (Millioni Mia Moja na Kumi na mbili) ambazo Feisal aliziweka katika Akaunti za Klabu.

Tunapenda kueleza kuwa, kuna taratibu na kanuni za Shirikisho la Soka la la Tanzania (TFF) na zile za Shirikisho la Mpira wa miguu Duniani (FIFA) ambazo ni lazima zifuatwe na timu yoyote ile inayotaka kumsajli mchezaji yeyote wa Klabu ya Young Africans SC (YANGA).

Yanga, inasisitiza kuwa, Feisal Salum Abdallah ni mchezaji halali ya Yanga na ana mkataba hadi kufikia Mei 30, 2024.

Imetolewa na Idara ya Habari
Young Africans Sports Club
Huu ndio msimamo wetu wananchi. Kumbe Azam anatumiwa tu na mama yake Kolo kumpata Fei. Tulichoamua tumemrejeshea fedha zake, tuna mute hadi dirisha dogo lifungwe kisha tunakaa mezani kuzungumza. Atalainika tu.
 
Hizo fedha katoa Azam, tunajua
 
Bado Yanga na masahabiki wao wanaamini mchezaji naye ni shabiki, mchezaji yuko kazini ikiwa analipwa milioni akapatikana mwajiri wa kutoa 3 lazima mtu atimke. Wanapooza tu upepo wa mashabiki kwa kuwadanganya eti milioni 112 imerudishwa kwa Feitoto, waweke na deposting slip hadharani ili tuamini. Wasiwadanganye mashabiki wao eti mazungumzo yalikuwa yanaendelea wakimshirikisha mamake Fei. Mamake FEI ndo hataki kuhama Fuoni na kwenda kuishi kwenye upepo tulivu wa FUMBA TOWN thubutu. Kina Ally Kamwe wajifunze kuheshimu wakubwa zao, leo aje basi awaambie mashabiki, wapenzi na wanachama wa Yanga kuwa FEI Kwenda Azam ataenda kupanda boat kwa ajili ya kwenda ZNZ lakini si kuchezea timu ya wauza ukwaju.
 
Ishi ya Haaland haiendani kabisa na hii acha kufananisha vitu.
Haaland Dortmund waliweka kipengele kua baada ya misimu 2 endapo itatokea timu itafikia paund mil 64 basi itamnunua na man city walitoa Hela pale sasa hii inafanana vipi na ishu ya Feisal alovunja mkataba?
 
Bado mkuu unaongea nadharia hiyo notice alitoa lini?
 
So dortmund hawajapata pesa yoyote toka kwa man city sababu ya hiyo release clause,jamaa uwa mnatumia akili kweli au mmetanguliza mapenzi,Yanga si kama haitaki fei aondoke ila taratibu zifuatwe,kama taratibu za release clause ndio ziko hivyo asubuhi tu mchezaji anaamka na kurudisha signing fee ingekua vurugu basi!
 
Ulianza na mazungumzo, umehamia kwenye notice. Yanga walijuaje kuwa hizo hela alizodeposit Fei ni kwa ajili ya kuvunja mkataba? πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ acha kuchekesha
Walijuaje bila notice? Haaa haaa
 
Ulianza na mazungumzo, umehamia kwenye notice. Yanga walijuaje kuwa hizo hela alizodeposit Fei ni kwa ajili ya kuvunja mkataba? πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ acha kuchekesha
Hivi unajielewa kweli?
Lazima kulikua na mazungumzo na ilipoonekana hayafiki popote ndo mtu huamua kufwata utaratibu wa kuvunja mkataba.
Sasa wewe maelezo yako hapo juu umedai unalipa Hela unasepa sasa ingekua hivo si kila mtu angesepa tu kazini akiona matakwa yake hayatimizwi.
 
Mkuu kuna barua nyingine tofauti na Ile iloandikwa ya tarehe 22 ?
 
... ingekua hivo si kila mtu angesepa tu kazini akiona matakwa yake hayatimizwi.
Hadi sasa ndivyo ilivyo kazini, unatoa notisi, unaweka mzigo unasepa. Hakuna haja ya mazungumzo. Ukiona mwajiriwa anafanya mazungumzo ujue huyo anatishia tu kuondoka.

Mazungumzo aliyafanya wakati ule hana nia ya kusepa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…