Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Felista Njau, ameibua mbinu mpya kwa kuacha mikutano ya hadhara na badala yake kuingia moja kwa moja masokoni, akiwafikia wakina mama na wafanyabiashara wadogo.
Njau, ambaye sasa ni sehemu ya timu ya kampeni za CCM, anasema mkakati huo unalenga kuwafikia makundi ambayo mara nyingi hayapati nafasi ya kuhudhuria mikutano ya kisiasa kutokana na majukumu ya kila siku.
“Wanawake hawa ndio uti wa mgongo wa familia zetu. Wengi wao wanaendesha familia kupitia biashara za sokoni, lakini mara nyingi wanakosa kusikiliza sera kwa sababu muda wao wote upo kwenye vibanda. Ndiyo maana nimeamua kuwafuata huku walipo,” alisema Njau wakati akizungumza na wafanyabiashara katika Soko la Kimochi, Moshi.