Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Muigizaji mashuhuri wa tamthilia ya Jua Kali, anayejulikana kama Femi, ameibuka na kutetea wanawake kutoka Mkoa wa Singida wanaofanya kazi ya uhudumu wa baa (baamedi), akieleza kuwa uwepo wao kwenye sekta hiyo unatokana na muonekano wao na mvuto wa kipekee unaosaidia kuvutia wateja.
Femi ameyasema hayo wakati akijibu mtazamo hasi na dhana zilizopo kwenye jamii dhidi ya wanawake wa Singida. Mbali na kutetea mchango wao kwenye biashara za baa, aliongeza kuwa wanawake kutoka mkoani humo pia wanapata fursa kwenye sekta mbalimbali za huduma na ukarimu, ikiwemo sekta ya usafiri wa anga kama wahudumu wa ndege.
"Sisi ni warembo, na waume zenu wanapenda wakija baa wanywe huku wanasafisha macho, sisi ni kivutio kwa sababu Singida ndo mkoa unaoongoza kutoa wanawake warembo... Wanawake kutoka Singida tukigomea kazi ya baamed, baa nyingi zitafungwa kwa kukosa wateja," alieleza Femi.
Muigizaji huyo alihitimisha kwa kusisitiza kuwa nafasi ya wanawake wa Singida kwenye sekta ya huduma ni kubwa, na bila ushiriki wao katika biashara za vinywaji na burudani, baa nyingi zingekabiliwa na ukosefu wa wateja.