KERO Feni na AC katika Majengo mengi ya Chuo cha DIT - Dar ikiwemo Maabara hazifanyi kazi

KERO Feni na AC katika Majengo mengi ya Chuo cha DIT - Dar ikiwemo Maabara hazifanyi kazi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Mnasomea technology, lecturers wenu wanashindwa kuwapa hizo AC na feni mtengeneze wenyewe?🤔
Nenda VETA unakuta mali zao chakavu. Ila itakuwa ni ile sheria ya manunuzi inawabana mpaka watangaze tenda.
 
Kwani Serikali ya Wanafunzi siku hizi haipo au hilo sio jukumu lao kupaza sauti!😂
 
Can't you get to apply the acquired skills on repairing those deformities, How dare you to Call DIT learners while failing to fix such minor issues?
Who gonna Be?
 
Kwani Serikali ya Wanafunzi siku hizi haipo au hilo sio jukumu lao kupaza sauti!😂
Juzi alikuja dogo wangu anasoma kwenye Chuo hicho analalamikia hiyo changamoto, swali langu la kwanza nikamuuliza Serikali ya Wanafunzi imewasaidiaje kupaza sauti, akasema majibu wanayopewa ni kwamba wanalifanyia kazi.

Ni kweli vijana wanateseka naamini kama limefika hapa jukwaani mamlaka zitawajibika kupunguza kero hii ikizingatiwa kipindi hiki ambapo kuna joto kali
 
Madarasa mengi na Maabara za Chuo cha DIT yana changamoto ambazo zinafanya tunashindwa kusoma tukiwa na utulivu, nazo ni; AC na feni nyingi hazifanyi kazi.

Mfano mimi ninasoma ETE, Jengo la mawasiliano kuna Maabara 4, zote hakuna AC wala feni tunapoingia kunakuwa na suffocation sana na joto kali sana, huu ni mwaka wa pili nimezikuta hivyo na hakuna jitihada zozote.

Upande wa majengo ya Block B na C Pia, mamlaka zilifanyie kazi hili tafadhali maana tunakuwa kama wafungwa na ada tunalipa, yaani hiki ni chuo cha Teknolojia (Dar es Salaam Institute of Technology - DIT) lakini tunakuwa na kero kama hizi ndogondogo, ni aibu kwetu.
Nunua feni Yako ndogo nenda nayo chuo Kuna socket hapo acha kupoteza muda watu wanakula urefu wa kambamba
 
Ni Taasisi, wala sio Chuo.
nweiiii wahusika watashughulika na hilo tatizo.
 
Chuo cha serikali kinacho zingatia wanafunzi kusoma bila mawazo ya Joto ni Law school tu nyie wengine jipepeeni
 
A
Can't you get to apply the acquired skills on repairing those deformities, How dare you to Call DIT learners while failing to fix such minor issues?
Who gonna Be?
natengeneza yeye alafu mafundi waliojiriwa wanakipwa mishaara
 
Back
Top Bottom