Kama Mkapa ametokea kuwa ni jambazi, sioni sababu kabisa kulaumu eti Nyerere ndiye aliyejua ujambazi wake huo na bado akaamua kumpigia kampeni kwa waTanzania ili wamchague.
Kwa mtu wa kawaida, nadharia kama hii haiingii akilini hata kidogo; lakini inapotokea kuwa wengi wetu tunakuwa na "Beautiful minds" basi hata udadisi kidogo inatuwia vigumu kuutumia.
1. Mwalimu alijua kuwa mkapa, ana kasoro ndio maana hakuwahi kumpa uwaziri mkuu hata mara moja kwa sababu hakumuamini, lakini ilipofikia urais akakumbuka kuwa aliwahi kuwa mwananfunzi wake Pugu.
2. Talking about nadharia na Mwalimu, na kukaa sawa je ile ya ku-support wizi wa uchaguzi wa visiwani, nayo imekaaje mkuu, sawa au sio sawa? au ni "ugly minds" kama sio beautiful minds?"
Hatuelezwi Nyerere alikuwa na mradi gani na huyu Mkapa licha ya kujua ubovu wake mwingi!
Je Mwalimu alikuwa na mradi gani na Mwinyi, tulishawahi kuelezwa? Maaana aliyemchagua si yeye mwalimu, au? NEC na cc ilimktalia Salim kuwa rais 1985, lakini ikampitisha kwa kura 90% kuwa mjumbe wake, is that a nadharia to you au beautiful minds?
Kama Mkapa ametokea kuwa ni jambazi, sioni sababu kabisa kulaumu eti Nyerere ndiye aliyejua ujambazi wake huo na bado akaamua kumpigia kampeni kwa waTanzania ili wamchague.
Hapana hoja iliyotolewa na mkuu mmoja huko nyuma ni kuwa Mkapa alimficha mwalimu makucha yake ya ujambazi, hilo ninakataaa kabisa ninasema kuwa mwalimu, alimjua vizuri Mkapa na tabia zake, lakini akaamua kwa makusudi kumpa urais anyways, na matokeo yake yameonekana na hasa serikali tuliyonayo sasa ambayo tulipewa na huyu huyu mkapa, sasa kama ni nadharia itakuwa ni ile ya mwanasheria wake mkuu wa mkapa kuwa na dola millioni moja US, na paunds millioni 5, UK labda hiyo kwako ni nadharia ya "beautiful minds" huku mshahara wa kima cha chini cha mwananchi ni dola kama $ 100 kwa mwezi, umeme ukiwa dola 50 kwa mwezi,
The rest ni hadithi za kawaida za apologist wa mwalimu, ukweli ni clear kuwa mkapa ni product ya mwalimu, kama alivyo muuungwana na Rostam, ni "product ya beautiful minds" ya mkapa. Wananchi we have to pay for this beautiful minds, lakini some of us bado tutasendelea kupiga kelele until the man akitinga mahakamani and he will tena very soon!
And again, waliotufikisha hapa tulipo as a nation sio wale ambao hawakuwahi kuwa marais, isipokuwa kina mkapa waliowahi kuwa, now lets talk about that tena in a serious note, sheria za jamhuri zinasema ni bodi ya wakurugenzi wa bandari ndio wenye mamlaka ya mwisho kuhusu tenda za bandari, lakini boom comes mr. Clean president na kuwaamuru wakurugenzi wa bandari kumpa Karamagi, 25 years of tenda ku-run containers za bandari yetu, unasema hizi ni nadharia zilziokaa sawa?
Tanzania tuna safari ndefu sana!