Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Fuatilia yanayojiri Bungeni leo tarehe 31 Januari, 2023 kwenye Mkutano wa Kumi, kikao cha kwanza.
HOJA YA SEHEMU ZA KUSUBIRI KUWAONA WAGONJWA
Mbunge wa Viti Maalum, Mariam Nassor Kisangi ameuliza kuhusu mpango wa Serikali katika kujenga na kuongeza maeneo ya kusubiri kuona wagonjwa katika hospitali Nchini.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt Festo Dugange alisema Serikali inaendelea na ujenzi wa hospitali katika halmashauri ambazo hazikuwa na huduma hiyo na kuwa tayari kuna hospitali 127 zinaendelea na ujenzi.
Amesema “Kumekuwa na changamoto ya maeneo ya kusubiri kuona wagonjwa katika hospitali nyingi, ili kutatua changamoto hiyo Serikali katika mwaka wa fedha 2023/24 imetenga bajeti ya Tsh. Bilioni 2.04 kwa ajili ya ujenzi wa sehemu za kusubiria wagonjwa katika zaidi ya hospitaili 100.
“Changamoto hiyo inazikumba Hospitali za Temeke, Amana na Mwananyamala Mkoani Dar es Salaam.”
MGAMBO KUSUMBUA WATU MUHIMBILI
Aidha, Mbunge huyo alihoji kuhusu tamko la Serikali kuhusu mgambo kufukuza wanaosubiri kuwaona wagonjwa katika Hospitali ya Muhimbili.
Naibu Waziri wa Afya, Naibu Waziri wa Afya Dr Godwin Mollel akajibu kuwa upande wa Hospitali ya Mwananyamala na Temeke kuna bajeti imetengwa kwa ajili ya ujenzi huo, kuhusu Muhimbili ujenzi unaendelea na ndani ya miezi mitatu kila kitu kitareje kama kawaida.
TATIZO MKOANI IRINGA
Mbunge wa Viti Maalumu, Rita Kabati amesema tatizo hilo ni kubwa Mkoani Iringa hasa katika Hospitali ya Mkoa, amedai kuwa wananchi wanalazimika kusubiri kuwaona wagonjwa kwenye maeneo ya magereza.
Akaongeza kuwa hata katika Wilaya ya Kilolo na Mufindi napo kuna changamoto hiyo, akaongeza “Kuna haja ya kuwepo kwa hosteli, wale wanaosubiri wagonjwa wawe wanalala nje ili kusubiri kuwaona wagonjwa.
Naibu Waziri wa Afya, Naibu Waziri wa Afya Dkt Godwin Mollel amesema kweli kuna changamoto hiyo na kumekuwa na hoja kuhusu kuihamisha hospitali hiyo lakini hilo halitawezekana kwa sasa kutokana na aina ya uwekezaji uliofanyika.
“Kuna mambo ya muhimu yanafikiriwa katiya TAMISEMI na Wizara ya Afya kabla ya kufanya maamuzi.”