Fid Q: Hakuna kitu rahisi kwa sasa kama kudata. Kwa haya ya BASATA ni wazi wasanii watadata sana

Leak

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2012
Posts
52,916
Reaction score
43,505
Kati ya wasanii ambao nawafatilia sana katika kila neno analo tamka kwenye muziki wake basi ni Msanii Fid Q.... maana kila atamkalo kwenye wimbo lina maana kama si leo basi ni kesho litakuwa lina maana zaidi....

Kwenye wimbo wa AY unaoitwa Microphone kuna msatari Fid q anasema"NDOTO haziwi mpaka USINGIZI ukiukata/ na hakuna KITU RAHISI kupata SIKU HIZI kama KUDATA••• "
Huu mstari unaongea mengi sana kuhusu sanaa na wasanii wenzie na ni ukweli usiopingika kabisa kuwa wasanii wetu ambacho cha haraka kwa sasa wanaweza pata ni kudata kabisa ndio maana unaona kila leo twasikia habari za wasanii kula madawa ya kulevya.

Sanaa imekosa muongozo kabisa si filamu wala muziki...wasanii wetu hawapati hela kama wanavyo jaribu kutuonesha kwenye mitandao ya kijamii na ukitaka kufahamu uhalisia wa wasanii wetu ni wakati wakikutwa na janga....mfano angalia kwa mzee majuto...

Kwa sanaa ilivyo na inavyo endeshwa na Basata kupitia Harrison Mwakyembe ni wazi kabisa wasanii wataendelea kuchanganyikiwa kwakuwa Basata chini ya Mwakyembe wameshindwa kuwasaidia kabisa ndio maana hadi sasa sintofahamu kuhusu kanuni mpya za Basata kuhusu sanaa na kila aliyesoma zile kanuni ni wazi kabisa atakubaliana nami kuwa kwa sasa wasanii kitu watakacho pata kwa urahisi ni kudata na si hela kwakuwa kwa zile kanuni hakuna deal watapata..

Kitu wanacho hitajika kukifanya kwa sasa hawa wasanii kwa sasa ni kuwa na umoja na kuwa na mambo ya kusimamia kwa pamoja lakini kinyume na hapo wataishia kudata...

Wasalaam
 
Wasanii wa bongo bwana!
Mwakyembe alishawahi Sema hata ukiwaita mkutane mjadili hawaji!

Ila wakishtushwa na hizo tozo ndo wanaibuka kama swala waliokurupushwa na simba!

Jana wameitwa viongozi wa vyama vyao kwenye XXL hakuna Hata la Maana wanaloongea!
 
Basata haijafikia level ya kuvuna toka kwa wasanii ,yenyewe ndo inapaswa iingize hela kwenye sanaa ikue after miaka ya uwekezaji ndo yaje mavuno,fatilia congo nchi ilipeleka wakongo wengi kijifunza ufaransa ikaweka hadi wizara ya muziki leo inavuna kwenye muziki kuliko nigeria na south ukizijumlisha sasa unatak umtoze harmonise jamani basata imejenga vipi uwanja wa kuzalisha kina harmonizer hadi iwavune very hopless
 


Wanasubiri uchaguzi 2020
 
Hawa wasanii acha waisome namba mpaka akili ziwakae sawa. Kwenye kampeni za uchaguzi wakipewa buku kumi tu wanakata viuno kama hawana akili nzuri
 
Lakini Steve aliongea la maana sana akasema wazi kabisa kuwa wasanii wanatakiwa kuungana na kuzingatia mambo ya msingi na wana matatizo mengi kuzidi waliyo nayo basata....wasanii tatizo hawana umoja halafu wengi wajauaji sana
 
Basata ni tatizo kabisa na katika hili namshangaa Mwakyembe
 
Wasanii wengi wana umaskini wa kujitakia, unakuta msanii ana followers kama 1Million kwenye social media zake, na hawezi kuwauzia watu 100,000 tu kazi yake ya sanaa, kimahesabu akiamua kuuza CD 1 kwa shilingi 2000 tu kwa watu 100,000 anapata 200,000,000. Kaz yao ni kulalamika tu.
 
hahahahaha hii nayo ni ya kufikirika
 
BASATA ni baraza la sanaa.

Hao Wasanii wamezoea kukatiza tu barazani na milegezo yao na visimu vya kupangusa...Wazee wamekaa barazani wamewaangaliaaaa....wakachanga akili wakaja na solution ya kuwakomesha.

Nikiwa kama mdau nashauri Wasanii walipe ili Baraza nalo lineemeke.
 
Malipo yaana anzia hapa hapa duniani kabla ya kwenda motton, hiyoo ndiyo ccm walio ipigia debe 2015, sasa imewageuka na bado!
 
Mkuu ukiachaga mambo ya Uccm unakuaga na akili sana....ila ukiingiza tu mambo yako yale ya nyundo na jembe sijui,unapuyanga mnoo😀😀
 
A
Acha kuleta comedy buraza.....hahahahah
 
Malipo yaana anzia hapa hapa duniani kabla ya kwenda motton, hiyoo ndiyo ccm walio ipigia debe 2015, sasa imewageuka na bado!
Kwani kuna kosa gani kuipigia debe CCM? wangeipigia debe Cuf?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…