Leak
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 52,916
- 43,505
Kati ya wasanii ambao nawafatilia sana katika kila neno analo tamka kwenye muziki wake basi ni Msanii Fid Q.... maana kila atamkalo kwenye wimbo lina maana kama si leo basi ni kesho litakuwa lina maana zaidi....
Kwenye wimbo wa AY unaoitwa Microphone kuna msatari Fid q anasema"NDOTO haziwi mpaka USINGIZI ukiukata/ na hakuna KITU RAHISI kupata SIKU HIZI kama KUDATA••• "
Huu mstari unaongea mengi sana kuhusu sanaa na wasanii wenzie na ni ukweli usiopingika kabisa kuwa wasanii wetu ambacho cha haraka kwa sasa wanaweza pata ni kudata kabisa ndio maana unaona kila leo twasikia habari za wasanii kula madawa ya kulevya.
Sanaa imekosa muongozo kabisa si filamu wala muziki...wasanii wetu hawapati hela kama wanavyo jaribu kutuonesha kwenye mitandao ya kijamii na ukitaka kufahamu uhalisia wa wasanii wetu ni wakati wakikutwa na janga....mfano angalia kwa mzee majuto...
Kwa sanaa ilivyo na inavyo endeshwa na Basata kupitia Harrison Mwakyembe ni wazi kabisa wasanii wataendelea kuchanganyikiwa kwakuwa Basata chini ya Mwakyembe wameshindwa kuwasaidia kabisa ndio maana hadi sasa sintofahamu kuhusu kanuni mpya za Basata kuhusu sanaa na kila aliyesoma zile kanuni ni wazi kabisa atakubaliana nami kuwa kwa sasa wasanii kitu watakacho pata kwa urahisi ni kudata na si hela kwakuwa kwa zile kanuni hakuna deal watapata..
Kitu wanacho hitajika kukifanya kwa sasa hawa wasanii kwa sasa ni kuwa na umoja na kuwa na mambo ya kusimamia kwa pamoja lakini kinyume na hapo wataishia kudata...
Wasalaam