Fideline Iranga amekuwaje?

Fideline Iranga amekuwaje?

Da kumbe kapona,Mungu ni mkubwa,Mungu akurudishie afya yako fide
 
Kwani ni yeye huyo SL? Amekuwa kimodeli kweli au alienda india kama Mustafa Hassanali labda...
Ni yeye! Aisee Mustapha nilivomuona kwa mara ya kwanza nilishtuka, nkawa namhurumia nikijua labda kaumwa ghafla na kisukari manake nacho kinakataga weight upesi, siku hizi ndo nimemzoea!
 
Hongera Fideline,umeonesha nini maana ya kuwa Role Model.
 
binafsi nampenda akiwa mnene kuliko alivyokonda, naona anapendeza zaidi akiwa alivyokuwa zamani kuliko alivyo sasa, unless picha zake za sasaivi hazikutoka vizuri ...... Pia kuhusu kukonda nadhani amefanya diet ya makusudi ili apungue, si mnajua yeye ni model yuko kwenye mambo ya fashion ambayo hayafagilii ubonge.

Watu mshaanza kum-judge kuwa mgonjwa, mmh jamani!! Wagonjwa wangapi ukiwaona ni wanene ile mbaya kutokana na madawa wanayokunywa ya kurefusha maisha? so, kukonda sio kuumwa jamani, ni maamuzi ya mtu kujiachia na ubonge au ku-diet apungue, dont judge her wrongly......
 
Tunaishi kwa definition za magharibi: kesho wazungu wakisema urembo ni ubonge atanenepeana kama michellin tena?
 
Kachukiza afadhali zamani,lakini ni uamuzi wake tuuheshimu.
 
Back
Top Bottom