Fiesta Dar yabumaaaaa watu wachache

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
20,137
Reaction score
26,189
Yani katika vitu vinavyowakosesha amani CLOUDS ni WCB.

Kiukweli tangu fiesta ianzishwe mpaka leo hakuna show mbovu kama show ya jana [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]yani watu walikuwa wachache sana mpaka wakashusha bei za tiketi lakini wapi hakuna aliyeingia mpaka wakaamua watu waingie bure lakini bado wakala za uso.

Clouds waliamua watu waingie bure ili angalau waonekane na wao walijaza ili waje kuvimbia WCB ,Ha ha ha ha daaah sijui walikuwa hawajui kwamba kizuri hujiuza kibaya chajitembeza .


Hiyo yote tisa kumi ni huyo anayejiita King , yani uharo mtupu show mbovu kupindukia mpaka hata clouds wameona aibu kumpost [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] .

Kuna haka kalikorubuniwa katoroke WCB kisa ananyonywa ,huyu ni miongoni mwa watu ambao wana majuto makubwa sana kwa sababu kila anachokifanya kinabuma na anazidi kufubaa tu kila kukicha ,angalia hata nguo alizovaa jana ,ni aibuuuuuuu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23].

Twende kwenye show sasa mpaka huruma angalau kidoooogo alipoimba Kokoro .


Clouds wamshukuru sana Chidibenzi angalau aliamsha amsha kidogo wengine wote chaliiiiiiiiii [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]


#HAWAAMINI WANACHOKIONA#

#SANAA IMEZALIWA UPYA#

#MCHEZO USIUCHEZEE WEWEE# KABISAAAAAAAA#.
 
Ngada sijui zina nini yaani mtu ata awe talent vipi lazima zitaharibu talent yake mf Darassa, ila Chid Benz bado ana fight ila jamaa kamsha jana alafu ana mapafu naona leo kila mtu ana mwongelea yy.Ila hiki kimachowakuta Clouds wakichukulie kama somo waache kugombana na wasanii.
 
Kwa ubovu na kubuma kwa show ya jana, clouds wana kazi kubwa kuendelea kuilinda brand ya Fiesta.

Fiesta ilikuwa show ya kuonyeshwa live kwenye tv leo hii hata picha za kawaida zinafichwa ili kuepusha aibu.

Watu sio wajinga wakiwapa hadhi ya kuwa radio ya watu mkaanza kuwapanda kichwani kesho wanaamia pengine na hawatorudi tena kwenu.

Mwaka unaokuja tutegemee maumivu zaidi upande wa clouds.

Wasafi tumieni makosa ya wenzenu kujifunza sababu mnaenda kuwa giants, watu wanawwza kuwa hawazungumzi hila hawapendi kufanyiana ubaya.
 
Maajabu ya pilipili kichaa katika mwili wa binadamu
LICHA ya muwasho, wataalamu wanasema pilipili kichaa ina faida mbalimbali katika mwili wa binadamu kwa kuwa ina ina uwezo wa kusaidia kwa kiwango kikubwa mtu asipate magonjwa makubwa manne.
 
Mipashoooo mingi!!
 
Fiesta ikifa ni watu wengi sana wataumia mbali na clouds, nilitegemea utataja makosa lakini pia utatoa hata mwanzo wa nini unadhani kifanyike

Mnaoshabikia kufa kwa Fiesta na Clouds ilhali mnaishabikia wasafi bhasi hamjielewi..monopoly wote duniani hawana tofauti katika kutaka super normal profits. Kushindwa kwa mavoko sio kitu cha kufurahia maana itafika kipindi wasanii wa WCB nao watakabwa shingo na kwa hofu ile ile ya kutotoboa bila WCB kama ilivyokuwa clouds..watanyonywa zaidi

Nachoona kuwe na Festivals mbalimbali ili nguvu ya wasanii iwe kubwa maana akikosa Fiesta ataenda wasafi au mziki mnene..hii ndo itakuwa solution
 
Tatizo CMG nao mashabiki wanapenda figisu figisu kila siku kuwa wao Hamna mtu alifanyiwa figisu kama Majizo mpaka akapumzika kufanya matamasha baadaye ndio akarudi na EFM.

Moja ya tukio waliomfanyia Majizo ni lile tamasha lake aliwaita Busy signal, Tpain, Joe Thomas leader club akalipigia promo zaidi ya mwezi mmoja imebakia wiki, CMG wanatangaza kumleta Fat Joe na Eve siku na tarehe moja kwenye viwanja vya Posta. Huwezi amini Majizo alikuwa hasara kubwa kwani watu walikuwa wachache sana, Jtatu Hando na Kibonde wakawa wanampiga vijembe vya mafumbo Majizo.

So huwezi jua hata hao Wasafi wanapitia nini, ila Wasafi nao fitina na uhuni wanajua na siku zote usipende kuwafanyia wenzio kile usichokipenda kufanyiwa ww.
 
Brother hizo figisu ni sehemu ya biashara ila ndo vile wabongo tumezoea biashara za kijamaa... walikuwa wanaua ushindani tu japo kwa upande wa jicho la kibinadamu ndo walifanya sio poa

WCB imekua kwa figisu na si ubora wa kazi zao pekee na ndo hivyo hivyo CMG ilikua pia.. wote wamekutana sehemu moja ila hofu ni moja tu Wasafi ikimuweka chini Clouds na yeye itafika kipindi atataka pesa zaidi maana atakuwa na nguvu...

Wanasema usiuamini uaminifu wa mtu mwenye njaa yaani ndo kama Wasafi kwa sasa maana wanatafuta njia tu ndo maana unawaona wapo hivyo japo dalili za kupenda kutawala kila kitu ni jadi ya WCB kama brand.. hivyo akheri Efm ndo angemuweka clouds chini kuliko wasafi ambao wana vinasaba vya CMG
 
Mbona nilimsikia shaffi ile ijumaa kuwa robo tatu ya tiketi zimeshauzwa!?
kushuka kwa clouds ni kumbeba sanaa mwenyekiti wa lumumba walijua clouds wanasikiliza Lumumba tu.
Waache wapotee
 
Hii imekaa kiushabiki zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…