FIESTA: Hii haikubaliki!

Ruta niliweka link original ya hiyo thread ya Compact na iliandikwa "usahili"....naona mod washarekebisha ila bado hoja yangu inasimama pale pale....naona hata link imeondolewa...
Si usahili... Ni usajili
 
LAbda wewe ndo upeo wa kufikiri mdogo.sio kweli kwamba upeo wetu wa kufikiri ni mdogo.acha dhana potofu mkuu
 
Wabongo bwana kwa kulalamika. Mtu kaandaa tamasha lake, kaweka terms and conditions ni hizi.
Ukitaka kushiriki unasaini mkataba hutaki unakaa pembeni.
Terms kaweka this time labda mtavaa mavazi yenye nembo ya mdhamini. Kama hutaki si unakataa just simple as that.
Badala ya kulalamika andaa tamasha lako unalohisi utaweka terms unazoona zinafaa.
 
Kwahiyo umefurahi kupotea kwao kwa kugoma kunyonywa? IPO siku walichokidai Leo kitawafaidisha wajukuu zao
Mkuu ebu nisaidie kidogo...mawingu wananyonya vipi wasanii..? Kitu gani wanachokidai hao wasanii ..?

Ni msanii gani alietoka hadharani akasema ananyoywa na je ananyonywa vipi...?
 
Mkuu inaelekea usikilizi radio j d alishaongea vyote
Mkuu...ukikaa ukaamua ufatilie hii kitu pande mbili za shillingi hakuna anae nyonywa..hawa walikua na ugomvi binafsi tu..na ugomvi wenyewe ulikua unamuhusisha mmliki wa radio, ndio akaamua nyimbo za jide zisipigwe...

Pia kwa Ruge na Sugu ilikua hivo hivo ugomvi binafsi..ila mmiliki akaamua ata nyimbo za Sugu zisipigwe pia...

Sitaki kuaamini eti wasanii wawili tu kwenye kundi la wasanii wengi tena maarufu na wenye nguvu ndo wameshituka wananyoywa...?

Kiba kafanya mziki kwa mda gani sijawai sikia hizi porojo eti ananyoywa, pia Byser Fid Joh na wengineo..

Jide na Rama dee wana matatizo binafsi na Ruge...hakuna cha kusema wananyoywa

Ni hayo tu mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…