Fiesta Mwanza: Wasanii wa Tanzania bado kuna namna jukwaani

Fiesta Mwanza: Wasanii wa Tanzania bado kuna namna jukwaani

Njoo 1ist Oct 2016 Escape One uone jinsi DIAMOND PLATNUMZ anavyopiga Live band ndio utajua tofauti,KUMBUKA LIVE BAND KESHAWAHI KUPIGA MARA NYINGI TU,ILA HII YA SASA NI MAPINDUZI YA LIVE BAND.
Ok nitaenda kwa heshima ya Diamond. Ila wakiweza kupiga kama p square live zao itakuwa bomba sana.
 
Sherehe zisizo na tija zimeshakataliwa na watu wameamriwa wafanye kazi na fedha wazitumie kwenye mambo muhimu sijui ni nani anaidhinisha kuandaa sherehe hizi za kihuni.
 
Nisicho kipenda kwenye fiesta hii ni clauz na basata kumtembeza msanii MAN FONGO akieneza upuuzi wa kiwango cha juu nchini et HAINAGA USHEMEJI hii kitu siipendi hadi kesho na kwa hili clauz na basata mjipange upya kwa sababu hii ni kinyume kabisa na maadili ya kitanzania.
hii inaboa sana sana
teh teh teh inaonekana huo wimbo unakupa machungu na una kukumbusha kitu usicho kipenda maishani mwako...
 
Fiesta ifutwe haina maadili zaidi ya kuchochea vitendo viovu kwa jamiii....
khaaaaa!!!fiesta imeanza 2001!
uovu hapa bongo umenza lini?

kuna kumbi km billz,diamond nk

kuna las vegas Casino,jolly club na match more vimeanza kabla ya fiesta!

hebu ulokole wenu pelekeni hukoooooo!!!!!!

imooooooooooo!!!!
 
Wanamuziki wa B 12 wamefeli. Unamuachaje mtu kama Darasa, Ney wa Mitego, Roma 2030, Kalla Jeremiah, Vanesa Mdee, Lady Jay Dee, Mayunga, Dully Sykes. Upopoma mtupu
Fiesta ya mwaka huu kama imefubaa sijaelewa tatizo ni nini.. Kuna watu wakikosa Fiesta uwezi pata matukio na hamsha hamsha.. Wamlipe vizuri Diamond anogeshe tour yao.. Darasa, God zila, mzee warioba, kalapina, Chid benz pia ni muhimu japo hawana hits ila shughuli yao nzito hao kina bilnas navy kenzo hawawezi kupiga show. Waache kubana matumizi watu wapate burudani
 
Jana kulikuwa na ufunguzi wa msimu wa fiesta , na mwamko wa watu ulikuwa mkubwa sana.

Changamoto kubwa ilikuwa kwa waandaaji hasa namna ya uchaguzi wa wasanii waliotumbuiza kuna baadhi ya wasanii hawakustahili kabisa kuwa kwenye jukwaa kubwa kama la jana mfano wasanii kama Nandi, Billnass walionyesha udhaifu mkubwa kulitawala jukwaa labda sababu ya uchanga wao.

Msanii Maua Sama alijitaidi kuimba live lakini bado hakuwa na vibe ya kutosha, aliimba cover nyingi labda kwa sababu ya uchache wa nyimbo zake mwenyewe.

Wasanii wakongwe kama Chege, Madee na Tundaman walijitaidi lakini amsha amsha haikuwa ya kutosha. Kulikuwa na wasanii wengi na tatizo kila msanii alikuwa anaimba nyimbo nyingi hadi inaboa.

Weusi ni moja ya watu wenye shangwe nyingi wanapopanda jukwaani lakini walikuwa na playlist mbovu ya nyimbo zao walishinda kuzipangilia kuleta hamasa.

Msanii mchanga Raymond alifanya vizuri sana alipata shangwe ya kutosha na alijitaidi kwenye connection na mashabiki, Baraka da prince nae alifanya vizuri akiwa nyimbani.

Alikiba alipanda kama suprise nae alifanya vizuri sana japo aliimba wimbo mmoja.

Waandaaji walishindwa kumanage muda Wizkid alipanda jukwaani saa kumi kasaro watu walishakuwa wamechoka ukizingatia walikuwa wamesimama muda mrefu. Wizkid aliimba live na band yake na alilitawala vizuri jukwaa alijiconnect vizuri na mashabiki wake alionyesha kwanini ni msanii star duniani.

NOTE: Wasanii wa Tanzania wanatakiwa kuanza kuimba live band kama tunataka mziki ukue zaidi. Wasanii wa Tanzania wamewekeza zaidi kwenye dancers kuliko kuimba.

Wizkid hakuwa na dancers lakini ile band yake ilijitosheleza kila kitu

View attachment 385166
Mkuu apo uko sawa kabisa kunasehemu anama , pichu ya manfongo mnato, Yani ni mbaya kabisa hii
Nisicho kipenda kwenye fiesta hii ni clauz na basata kumtembeza msanii MAN FONGO akieneza upuuzi wa kiwango cha juu nchini et HAINAGA USHEMEJI hii kitu siipendi hadi kesho na kwa hili clauz na basata mjipange upya kwa sababu hii ni kinyume kabisa na maadili ya kitanzania.
hii inaboa sana sana
 
Inakuaje watu wameimba ad nyimbo za kushilikishwa afu king anaimba wimbo 1 wakati anazo nyingi 2 izi dhalau
 
Kiukweli mimi nimeenda haya matamasha ya bongofleva ila sijaona bado wakunishawishi nirudi kumuona kwa mara ya pili zaidi ya lady jaydee. Labda mwenzangu uniambie ni bongofleva yupi anaefanya vizuri kwenye live band nikamshuudie na mimi.
Mkuu ulikuwepo kwel au umeadithiwa
nlicheka sana wizkid alivyopanda watu waliposhindwa kuitikia hata nyimbo1 jaman kukaw kam hakuna watu daaah kilengesa hii inatesa wengi sana
 
Nisicho kipenda kwenye fiesta hii ni clauz na basata kumtembeza msanii MAN FONGO akieneza upuuzi wa kiwango cha juu nchini et HAINAGA USHEMEJI hii kitu siipendi hadi kesho na kwa hili clauz na basata mjipange upya kwa sababu hii ni kinyume kabisa na maadili ya kitanzania.
hii inaboa sana sana
mkuu pole kwa kuchapiwa mkeo mziki ni burudani
 
Sherehe zisizo na tija zimeshakataliwa na watu wameamriwa wafanye kazi na fedha wazitumie kwenye mambo muhimu sijui ni nani anaidhinisha kuandaa sherehe hizi za kihuni.

sasa we hauoni hao wasanii wanafanya kazi na pesa tunayolipa kiingilio ndo inalipa kodi acha ukoloni
 
Back
Top Bottom