Yeah Egypt ni timu nzuri sana ila kwa mara nyingine Howard Webb anatoa maamuzi ya kutatanisha. In the first place it was a clear penalty but Webb pointed for a corner kick, then baada ya kuwasiliana na assistant ambaye sio among the referee assistants (washika vibendera) anabadilisha uamuzi jambo ambalo linakera na kuhoji credibility ya huyu refa. Tunakumbuka ni huyu huyu aliwapa Man Utd penati dhidi ya Spurs Man wakiwa nyuma 2-0, then wakashinda 5-2, kesho yake akaomba msamaha!
I do agree ni penati 100% alishika mpira ila uamuzi wa awali wa referee alisema ni kona jambo ambalo lingefanyika immediately kama yule mchezaji wa Misri asingejifanya kaumia na ndio maana wabrazil walilalamika sana hasa Lucio wakimuonyesha refa kwamba yule bwana alishika. Then baada ya slow mo replays yule msaidizi aliona lile tukio thru video akamtonya ref kwamba lile ni tuta. Hoja hapa sio kwamba ile ni penati au sio penati, ni suala la waamuzi kutumia video kuamua jambo, FIFA hawaentertain matumizi hayo katika kufanya decisions.Lakini si kashika, so justice has been done.
I do agree ni penati 100% alishika mpira ila uamuzi wa awali wa referee alisema ni kona jambo ambalo lingefanyika immediately kama yule mchezaji wa Misri asingejifanya kaumia na ndio maana wabrazil walilalamika sana hasa Lucio wakimuonyesha refa kwamba yule bwana alishika. Then baada ya slow mo replays yule msaidizi aliona lile tukio thru video akamtonya ref kwamba lile ni tuta. Hoja hapa sio kwamba ile ni penati au sio penati, ni suala la waamuzi kutumia video kuamua jambo, FIFA hawaentertain matumizi hayo katika kufanya decisions.
KOMBE LA MABARA 2009-CONFEDERATION CUP 2009
UJANJAUJANJA WA MISRI SAFARI HII WAKWAMA
Katika mchezo kati ya Misri na Brazil ambapo matokeo yalikuwa Brazil 4 vs Misri 3 ujanjaujanja wa wachezaji wa Misri ulikwama.Kwa miaka mingi wa-Misri wamekuwa wanakera wapenzi kwa visa vyao vya kujiangusha, kupoteza wakati wakijifanya wameumia hasa wakiwa wanaongoza kwa magoli.
Katika mchezo huu Al Muhamad alijiangusha na kujishika usoni akijidai ameumia vibaya kumbe kazuia mpira kwa mkono usiingie..baada ya ushauri wa refa aliyoko nje apewa kadi nyekundu.
Wamisri wamekuwa wakibebwa mara nyingi na CAF kwa vile makao makuu ya CAF yapo Cairo na waamuzi wengi wamekuwa wanaogopa vinginevyo hawatachaguliwa kuchezesha mechi za CAF hivyo kukosa mapato.
Misri sasa wanakata rufaa dhidi ya penati ya Brazil...kisa..kwa nini muamuzi alibadilisha mawazo baada ya kushauriwa na muamuzi wa akiba baada ya kuona video.
Nachotaka kuwaambia ndugu zetu wa Misri ni kwamba katika michezo mikubwa ya kidunia uwanjani kuna kamera chungu nzima kutoka kila upande..hilo wanalijua ...ujanjaujanja haukubaliki, ndio maana waamuzi wanavaa earphone na vifaa vingine vya hi-technology vinatumika hilo ndilo soka la leo...Nawashauri Egypt kama kweli wao ni bigwa wacheze mpira safi na sio kupoteza wakati na kuwanyima mashabiki raha..Mechi yao na Italy waonyeshe umahiri wao kimchezo ili kudhihirisha ni mabigwa wa Africa.
Swali kwa wapenzi wa mpira wa JF:Je sheria zinaruhusu muamuzi kubadili mawazo baada ya kupokea ushauri kutoka kwa mwamuzi wa nje?
Wow!Mechi ya Egypt na Italy itakuwa nzuri sana.
Ebana Egypt wako juu, kiwango chao nimekikubali