FIFA kufuta magoli yanayofungwa kupitia mpira unaotemwa na kipa

FIFA kufuta magoli yanayofungwa kupitia mpira unaotemwa na kipa

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,040
Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) linatafakari kufanya mabadiliko makubwa katika sheria ya upigaji penalti kwa kuondoa mabao yanayofungwa kupitia mpira unaotemwa na kipa.

Katika mapendekezo hayo, mchezaji atakuwa na nafasi moja pekee ya kufunga; endapo atakosa, mchezo utaendelea kwa kipa kuanzisha mpira kwa kutupa au kupiga.

1759141201398.png


Hatua hiyo inalenga kurahisisha maamuzi ya marefa na pia kuwapa walinda milango nafasi kubwa zaidi ya kujiamini.

Mwenyekiti wa kamati ya marefa wa FIFA, Pierluigi Collina ndiye kinara wa wazo hilo, akisema litapunguza utata kwenye maamuzi. Hata hivyo, bado kuna utata kuhusu kinachotokea iwapo mpira ukigonga mwamba bila kuguswa na kipa.

Iwapo litaidhinishwa, pendekezo hilo litaanza kutumika msimu wa 2026/27, jambo litakalofanya Kombe la Dunia la 2026 kuwa la mwisho kuchezwa kwa mfumo wa sasa wa penalti.

Chanzo: Mwananchi updates
 
Dah? Ata Mimi ntaenda kudaka golini imladi niuteme tu au siyo hata nikuungusa tu😃
 
Watz mna shida sana vichawani ndio maana CCM haitoki madarakani watu wanaumiza vichwa kuleta mabadiliko mpira uwe wa haki nyie mnapiga porojo ......VAR,sheria ya offside goal technology zote ni idea za kuondoa uonevu
 
Wabadilishe na sheria ya kuotea, ili mchezaji ahesabike ameotea awe amezidi mwili mzima tofauti na sasa hata ukizidi mguu tu ni Offside.
 
Hapo kwenye kugonga mwamba ndio kuna kipengele mfano mpira unagonga mwamba na kurudi uwanjani inakuaje?
 
Ni kuharibu mpira, raha ya mechi ni ugumu sasa kufanya mambo yawe mepesi mepesi ni kuharibu burudani ya mpira.
 
Back
Top Bottom