FIFA kuruhusu timu kuwa na wachezaji 26 Kombe la Dunia

FIFA kuruhusu timu kuwa na wachezaji 26 Kombe la Dunia

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
1656053881192.png

Shirikisho la Kandanda duniani Fifa limepitisha mpango wa kila timu kutumia kikosi cha majina 26 kwenye fainali za Kombe la Dunia Qatar 2022.

Itakumbukwa ongezeko hilo linakuja baada ya hapo awali kila timu ilitakiwa kuthibitisha majina ya wachezaji 23 kwenye kikosi chake lakini sasa kutokana na changamoto za virusi vya Corona imeisukuma Fifa kupitisha idadi ya wachezaji hao.

Kutokana na ongezeko hilo, Fifa pia imesema kuwa idadi ya wachezaji 15 watakuwa wanatajwa kwa ajili ya kukaa akiba ambayo ni idadi sawa na wachezaji wote 26.

Timu zote zinatakiwa kupeleka majina ya wachezaji ambao watashiriki michuano hiyo itakuwa Octoba 20, siku 30 kabla ya kuanza mchezo wa kwanza.
 
Back
Top Bottom