FIFA yalaani mchoma nyama kulishika kombe la dunia

FIFA yalaani mchoma nyama kulishika kombe la dunia

Ujinga mtupu

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2017
Posts
887
Reaction score
2,010
Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA limelaani kitendo cha mpishi maarufu duniani Nusr Et maarufu Salt Bae ambaye huchoma nyama na kuwalisha mastaa wakubwa duniani kulishika kombe la dunia siku ya Jumapili ambapo Argentina iliibuka bingwa.

Mchoma nyama huyo tajiri aliingia sehemu ya Uwanjani kujumuika na wachezaji kushangilia ushindi ambapo alipiga picha na nyota mbalimbali akiwemo Messi na Di Maria na ndipo alipopata fursa ya kulishika kombe wakati ambao Wachezaji wanafurahi nalo na kupiga picha.

FIFA imelaani kitendo hicho ikisema kombe hilo linapaswa kushikwa na wachezaji walioshinda na watu maalum waliopitishwa na FIFA hivyo mtu hata awe maarufu vipi sio kigezo cha kulishika kombe.

NB: Nikukumbushe hata lilipopita Tanzania kama ulivyo utaratibu wa FIFA kulipitisha kombe nchi mbalimbali kabla halijaenda kwenye nchi inayofanyika mashindano aliyepitishwa kulishika ni Rais Samia pekee wengine walipiga nalo picha likiwa ndani ya chumba chake cha box la kioo.
 
Jamaa Huyo
1671620486687.jpg
 
Back
Top Bottom