Unamfahamu maxrioba? Jamaa ni multi talented as anafanya vitu vingi katika ubora lakini sikutegemea kama angerudia kosa lile lile linalofanywa na bongomuvi wengi. Ana series yake inaitwa WE MEN, wengi tulitegemea utofauti wa mambo mengi ambayo kiukweli kajitahidi sana ingawa amefanya kosa lile lile la kuchagua wasichana sijui kwa kigezo cha uzuri au lah, kati ya waigizaji wake wote wa kike nafikiri ni Wema Sepetu tu ndiye anayeweza kuingiza vizuri (japo mi si mshabiki wake siwezi kukataa ukweli kuwa wema anajitahidi sana katika kuigiza) Wengine aliowarecruit ni tatizo sana, very fake, wamekosa kuwa natural kwenye kuigiza wanakera na kuboa, na yupo kaka mmoja mweupe hivi naye ni tatizo sana. Ukiwaangalia uigizaji wao ni kama kuna ombwe fulani hivi kwenye actions, ni kama kuna muda muigizaji hajui chakufanya....
Hivi wenzetu waliofanikiwa katika movie industry wanawezaje “kuigiza bila kuigiza”? Hii inasababishwa na waigizaji wenyewe au Directors?
Bongo tuna kosea sana,wasichana wa bongo movie walio ingia kuanzia 2010 mpaka hivi sasa 95% hawajui kuigiza ila uzuri wao ndio umewapa nafasi ktk tasnia hii.
Sasa hivi napo wamejaza mashombe shombe upande wa wanaume wanakazi ya kuuma lipsi na wengine kuanika vifua vyao.Hapo sio kwamba waigizaji wenye vipaji hawapo,wapo wengi tena wengine wapo tayari hata kuigiza bure ile ndio vile,wataambiwa hawana mvuto.
Angalia movie hizi za Captain Phillips,Tear of the sun,Blood Diamond wangalie waigizaji wake kutoka Afrika wa kawaida lkn wanavaa uhusika,nenda Nigeria waigizaji wao wa kawaida tu nenda South Afrika waigizaji wa kawaida ila wana vipaji.Sisi tunaangalia sura makalio,hips,vifua,ushombeshombe na six pack.
Mwisho wa siku tasnia inakosa ubunifu sababu wahusika hawana vipaji.Hizi tamthilia mimi huwaga naishia kuangaliaga promo ila sioni kitu kabisa.
Wanakazi tu ya kuuza sura ili wapate madanga,kesho waanze kugombania madanga.Asikudanye mtu mtu mwenye talent ataendelea kuwa bora na swala la ubunifu kwale lipo kwenye damu.
Mimi bongo movie huwaga si walaumi sana upande wa quality najua bajeti zao ndogo ila nawalaumu upande wa wahusika wao,siku hizi wengi wana kazi ya kuonyeshea makalio,hipsi na sura zao kuliko vipaji vyao,tasnia imekuwa ya kimalaya malaya kama danguro vurugu tupu na mimi nahisi kwa asilimia kubwa kuna rushwa za ngono humu ktk kutafuta vipaji.