Mkuu
Aggrey86,
Pole kwa kuuguliwa,
Tatizo la figo kujaa maji (Hydronephrosis) ..kitaalamu, haimaanishi tu figo kujaa maji bali pia kupanuka/kutanuka kwa njia ya taka mwili(mkojo) yaani katika figo yenyewe, kutoka katika figo na mirija inayotoa taka mwili hii kupeleka katika kibofu cha mkojo.
Binadamu wa kawaida ana figo mbili(upande wa kulia na wa kushoto katika eneo la tumbo). Hizi husaidia katika kaxi nyingi mwilini, Kutoa taka mwili, Kurutubisha/kutengeneza vichochezi(hormone), Kusaidia katika utengenezwaji wa damu, kuchuja sumu n.k.
Matatizo ya figo:
Kuna aina nyingi ya matatizo ya figo mfano maumbile, uwepo wake katika sehemu isiyo ya kawaida, Infection, Kujaa maji n.k.
Kujaa maji kwa figo:
Hapa hutokana na sababu kuu zifuatazo;
1 . Njia ya taka mwili(Mkojo) kuziba (yaani Obstruction): Ingawa sehemu tatizo hili linaweza kutokea sehemu yeyote katika njia kuu, mara nyingi/kwa asilimia kubwa hutokea katika sehemu figo inapoungana na mija(ureter) na sehemu nyingine ni pale mrija unapoungana na kibofu cha mkojo.Visababishi;
-Mawe(Kidney stones)
-Kuvia kwa bonge/vibonge vya damu(Blood clot)
-Saratani n.k
2. Taka mwili(mkojo) kurudi ilipotoka(Reflux): Hii hutokana na kuwepo kwa mgandamizo wowote katika mirija(Ureters) inayoleta mkojo katika kibofu.Mgandamizo huu husababisha kuwepo kwa msukumo(pressure) unaosababisha mkojo kurudi katika figo na kutoelekea katika kibofu. Uelekeo huu(Backflow) husababisha taratibu kutokea kwa tatizo.Visababishi;
-Saratani
-Mimba(Ujauzito)..hasa ujauzito mkubwa, mf. Mapacha, mtoto mkubwa n.k..lakini pia wakati wa ujauzito mabadiliko ya vichochezi(hormone) hufanya kushindwa ku-contract kwa usawa, kwa mirija.
Njia za kujikinga:
Asilimia kubwa ya watu wenye matatizo ya figo kujaa maji huwa na tatizo la kuwepo kwa mawe/vijiwe(Kidney stones). Haya "mawe" yapo ya aina mbalimbali na kwa namna yake(type) huweza kusababisha matatizo kama nilivyokwisha kusema. Mawe haya hutokana na vyakula tunavyovitumia.Vyakula vya protini nyingi, vyenye sukari na chumvi nyingi/kwa wingi. Vyakula vyenye madini mengi ya Sodium, Calcium, Phosphate n.k. Hapa ninamaanisha Samaki, Nyama, Chocolates, baadhi ya mboga za majani, dagaa, smoked foods, n.k endapo vitatumiwa bila usawa(Unbalanced diet).
Dalili:
Maumivu makali ya tumbo, kichefu chefu, kutapika, kutopata haja ndogo(mkojo), kukojoa damu, n.k
Matibabu:
Hutegemea umri, aina ya tatizo(yaani chanzo) hasa kutokana na vipimo.
Njia nzuri ya kujikinga ni;
-Kuboresha mlo wako.
-Kutumia maji mengi/maji kwa wingi.