Its Jensen
Member
- Mar 30, 2023
- 14
- 18
Habari wana Jamii forum, natumaini mko salama kabisa mnapambana kutafuta ugali
Sasa hivi kumekua na wimbi kubwa la vijana ambao wanaingia kwenye biashara, baada ya kukosa ajira walizokua wanategemea baada ya kumaliza masomo yao, walio fukuzwa kazi, na wengine ambao wanatamani kujiajiri ili kujikwamua kimaisha
Vijana wengi kwa sasa wamekua wakiingia kwenye biashara huku wakiwa hawana elimu ya kutosha kuhusu biashara wanazoanza kufanya, hii inasababisha biashara nyingi kufa ndani ya miezi mitatu ya mwanzo
Leo wakati nipo kariakoo naenda kutafuta nguo za watoto wangu za pasaka, nilikutana na rafiki angu mmoja ambaye nilisoma nae kidato cha 5 mwaka 2011 ambaye kwa sasa anamiliki biashara ya kuuza nguo hapa kariakoo.
Kipindi anafungua duka lake, kama alivyokua anajua biashara ili ipendeze ni kutafuta lango ambapo linaonekana vizuri ili wateja wengi wapate kumuona. Alifungua duka lake kwenye eneo lenye watu wengi ili aweze kuvutia wateja wengi.
Mwanzo kipindi anaanza alikua anauza vizuri, mzigo unatembea haswa , akawa na wateja wengi mpaka mikoani. Hata hivyo, baada ya muda mfupi, alianza kukosa wateja . Biashara ikaanza kuyumba , mzigo tena hautembei kama zamani.
Alianza kufikiria vitu vingi kwa nini biashara yake inakosa wateja wengi kama zamani. Alitafakari kwa muda mrefu na kugundua sababu kadhaa za tatizo hilo. Kwanza,alifikiri labda bei za bidhaa zake zilikuwa ghali zaidi ukilinganisha na duka lingine linalouza nguo za aina hiyo. Pia, aligundua kuwa bidhaa zake hazikuwa za ubora sawa. Bidhaa nyingine zilikuwa nzuri lakini nyingine hazikuwa na ubora wa kutosha.
Pia aliwaza kuwa hakuwa akifanya masoko ya kutosha. Alidhani kwamba kufungua duka lake tu lingetosha kuvutia wateja, lakini hakuwa akifanya matangazo ya kutosha. Hivyo, watu hawakuwa na habari za kutosha kuhusu duka lake.
Baada ya kugundua sababu za tatizo hilo, mmiliki wa biashara alianza kupunguza bei za bidhaa zake ili ziweze kuwa za ushindani. Alishughulikia suala la ubora wa bidhaa kwa kuhakikisha kuwa ananunua bidhaa bora kutoka kutoka china yeye mwenyewe, lakini biashara yake ikawa bado imegoma
Kumbe tatizo haikuwa hayo yote aliyokua akiwaza ila kuna mfanyabiashara mwenzake alimuwekea vitu kwenye mlango wake kwa juu, wateja wakija kwake wanaona duka la jirani yake, swala la biashara bila maelekezo kwa kweli ni gumu sana, kwa kijana yoyote ambaye ana anza biashara hakikisha unapata maelekezo kwanza, hakuna mtu atakayefurahia akikuona wewe unauza sana
Haijalishi ni rafiki ako wa namna gani, biashara haina urafiki, muombe sana mungu akusimamie pia kumbuka kufanya maelekezo ni muhimu sana, ukutazama biashara za watu wengi zinakua ghafla na kufa ghafla , sio kwamba hawajui biashara ila ni vile binadamu hatupendani na hatutaki kuona mwingine akifanikiwa