Fikirisha ubongo Unapoambiwa fanya utafiti kwanza kabla ya kufungua biashara

Fikirisha ubongo Unapoambiwa fanya utafiti kwanza kabla ya kufungua biashara

Its Jensen

Member
Joined
Mar 30, 2023
Posts
14
Reaction score
18
Habari wana Jamii forum, natumaini mko salama kabisa mnapambana kutafuta ugali

Sasa hivi kumekua na wimbi kubwa la vijana ambao wanaingia kwenye biashara, baada ya kukosa ajira walizokua wanategemea baada ya kumaliza masomo yao, walio fukuzwa kazi, na wengine ambao wanatamani kujiajiri ili kujikwamua kimaisha

Vijana wengi kwa sasa wamekua wakiingia kwenye biashara huku wakiwa hawana elimu ya kutosha kuhusu biashara wanazoanza kufanya, hii inasababisha biashara nyingi kufa ndani ya miezi mitatu ya mwanzo

Leo wakati nipo kariakoo naenda kutafuta nguo za watoto wangu za pasaka, nilikutana na rafiki angu mmoja ambaye nilisoma nae kidato cha 5 mwaka 2011 ambaye kwa sasa anamiliki biashara ya kuuza nguo hapa kariakoo.

Kipindi anafungua duka lake, kama alivyokua anajua biashara ili ipendeze ni kutafuta lango ambapo linaonekana vizuri ili wateja wengi wapate kumuona. Alifungua duka lake kwenye eneo lenye watu wengi ili aweze kuvutia wateja wengi.

Mwanzo kipindi anaanza alikua anauza vizuri, mzigo unatembea haswa , akawa na wateja wengi mpaka mikoani. Hata hivyo, baada ya muda mfupi, alianza kukosa wateja . Biashara ikaanza kuyumba , mzigo tena hautembei kama zamani.

Alianza kufikiria vitu vingi kwa nini biashara yake inakosa wateja wengi kama zamani. Alitafakari kwa muda mrefu na kugundua sababu kadhaa za tatizo hilo. Kwanza,alifikiri labda bei za bidhaa zake zilikuwa ghali zaidi ukilinganisha na duka lingine linalouza nguo za aina hiyo. Pia, aligundua kuwa bidhaa zake hazikuwa za ubora sawa. Bidhaa nyingine zilikuwa nzuri lakini nyingine hazikuwa na ubora wa kutosha.

Pia aliwaza kuwa hakuwa akifanya masoko ya kutosha. Alidhani kwamba kufungua duka lake tu lingetosha kuvutia wateja, lakini hakuwa akifanya matangazo ya kutosha. Hivyo, watu hawakuwa na habari za kutosha kuhusu duka lake.

Baada ya kugundua sababu za tatizo hilo, mmiliki wa biashara alianza kupunguza bei za bidhaa zake ili ziweze kuwa za ushindani. Alishughulikia suala la ubora wa bidhaa kwa kuhakikisha kuwa ananunua bidhaa bora kutoka kutoka china yeye mwenyewe, lakini biashara yake ikawa bado imegoma

Kumbe tatizo haikuwa hayo yote aliyokua akiwaza ila kuna mfanyabiashara mwenzake alimuwekea vitu kwenye mlango wake kwa juu, wateja wakija kwake wanaona duka la jirani yake, swala la biashara bila maelekezo kwa kweli ni gumu sana, kwa kijana yoyote ambaye ana anza biashara hakikisha unapata maelekezo kwanza, hakuna mtu atakayefurahia akikuona wewe unauza sana

Haijalishi ni rafiki ako wa namna gani, biashara haina urafiki, muombe sana mungu akusimamie pia kumbuka kufanya maelekezo ni muhimu sana, ukutazama biashara za watu wengi zinakua ghafla na kufa ghafla , sio kwamba hawajui biashara ila ni vile binadamu hatupendani na hatutaki kuona mwingine akifanikiwa
 
Biashara bila madhabahu hutoboi, chagua upande na uwe deep seriously, aidha utumie madhabahu ya mganga au ya MUNGU wa kweli, hapo ndio utoe sadaka na fungu la kumi.

Nb. Upande wa giza mwisho wake ni mbaya.
 
Hapo aya ya mwisho ndio kuna point ya msingi sana.
Habari wana Jamii forum, natumaini mko salama kabisa mnapambana kutafuta ugali

Sasa hivi kumekua na wimbi kubwa la vijana ambao wanaingia kwenye biashara, baada ya kukosa ajira walizokua wanategemea baada ya kumaliza masomo yao, walio fukuzwa kazi, na wengine ambao wanatamani kujiajiri ili kujikwamua kimaisha

vijana wengi kwa sasa wamekua wakiingia kwenye biashara huku wakiwa hawana elimu ya kutosha kuhusu biashara wanazoanza kufanya, hii inasababisha biashara nyingi kufa ndani ya miezi mitatu ya mwanzo

Leo wakati nipo kariakoo naenda kutafuta nguo za watoto wangu za pasaka, nilikutana na rafiki angu mmoja ambaye nilisoma nae kidato cha 5 mwaka 2011 ambaye kwa sasa anamiliki biashara ya kuuza nguo hapa kariakoo.
kipindi anafungua duka lake, kama alivyokua anajua biashara ili ipendeze ni kutafuta lango ambapo linaonekana vizuri ili wateja wengi wapate kumuona. Alifungua duka lake kwenye eneo lenye watu wengi ili aweze kuvutia wateja wengi.

mwanzo kipindi anaanza alikua anauza vizuri, mzigo unatembea haswa , akawa na wateja wengi mpaka mikoani. Hata hivyo, baada ya muda mfupi, alianza kukosa wateja . Biashara ikaanza kuyumba , mzigo tena hautembei kama zamani.

Alianza kufikiria vitu vingi kwa nini biashara yake inakosa wateja wengi kama zamani. Alitafakari kwa muda mrefu na kugundua sababu kadhaa za tatizo hilo. Kwanza,alifikiri labda bei za bidhaa zake zilikuwa ghali zaidi ukilinganisha na duka lingine linalouza nguo za aina hiyo. Pia, aligundua kuwa bidhaa zake hazikuwa za ubora sawa. Bidhaa nyingine zilikuwa nzuri lakini nyingine hazikuwa na ubora wa kutosha.

pia aliwaza kuwa hakuwa akifanya masoko ya kutosha. Alidhani kwamba kufungua duka lake tu lingetosha kuvutia wateja, lakini hakuwa akifanya matangazo ya kutosha. Hivyo, watu hawakuwa na habari za kutosha kuhusu duka lake.

Baada ya kugundua sababu za tatizo hilo, mmiliki wa biashara alianza kupunguza bei za bidhaa zake ili ziweze kuwa za ushindani. Alishughulikia suala la ubora wa bidhaa kwa kuhakikisha kuwa ananunua bidhaa bora kutoka kutoka china yeye mwenyewe, lakini biashara yake ikawa bado imegoma

kumbe tatizo haikuwa hayo yote aliyokua akiwaza ila kuna mfanyabiashara mwenzake alimuwekea vitu kwenye mlango wake kwa juu, wateja wakija kwake wanaona duka la jirani yake, swala la biashara bila maelekezo kwa kweli ni gumu sana, kwa kijana yoyote ambaye ana anza biashara hakikisha unapata maelekezo kwanza, hakuna mtu atakayefurahia akikuona wewe unauza sana

Haijalishi ni rafiki ako wa namna gani, biashara haina urafiki, muombe sana mungu akusimamie pia kumbuka kufanya maelekezo ni muhimu sana, ukutazama biashara za watu wengi zinakua ghafla na kufa ghafla , sio kwamba hawajui biashara ila ni vile binadamu hatupendani na hatutaki kuona mwingine akifanikiwa
 
Biashara bila madhabahu hutoboi, chagua upande na uwe deep seriously, aidha utumie madhabahu ya mganga au ya MUNGU wa kweli, hapo ndio utoe sadaka na fungu la kumi.

Nb. Upande wa giza mwisho wake ni mbaya.
Fungu la kumi waile matapeli wachungaji!?, bora kwa waislam zaka wanawapa maskini
 
Mkuu kuna levo ambayo ukisha fikia huko hata mchawi hakusogelei maana anajuwa kabisa ukimgunduwa tu habari yake na uchawi wake na yeye mwenyewe ndio mwisho

nahii nikwa sababu nguvu ya pesa nikubwa kuliko uchawi wenyewe
Matajiri ndio wanaongoza kwa kutoa kafara, Biashara ni fumbo kubwa
 
Back
Top Bottom