Filamu: Mwili wa mwanamke aliyekufa kwa sumu, umepotea Mochwari

Filamu: Mwili wa mwanamke aliyekufa kwa sumu, umepotea Mochwari

Script writers wa thrillers wa hii miaka hawana jipya.

Labda science finctions.

Kama ulipitia the coffin from hongkong ya hadley chase huwez zimia hii film.
 
Utafanya nini kama umefiwa, umeupeleka mwili wa mpendwa wako kuhifadhiwa alafu unapigiwa simu kwamba mwili hauonekani? Umepotea? Haujulikani ulipo?

Tafuta popcorn, ambaa na kisa hiki..

Baada ya kutokea ajali, mlinzi wa hospitali akigongwa na gari mita kadhaa kutoka eneo lake la kazi, inspekta wa polisi aitwaye Jaime anaitikia wito wa kuja kufanya upelelezi wa kesi hii yenye utata.

Anapofika hospitali anabaini mambo mawili, moja - mlinzi alidakwa na kamera akiwa anakimbia kwa papara kutoka eneo lake la kazi, mochwari, huku kinachomkimbiza hakionekani.

Na kukimbia huko ndo' kukampelekea aingie barabarani alipogongwa vibaya kiasi cha kulazwa akiwa hana fahamu mpaka sasa.

Pili - mochwari alipotokea mlinzi huyo kuna mwili wa mwanamke hauonekani, haijulikani mwili huo umeelekea wapi na ni nani aliyeuchukua!
View attachment 2958960

Inspekta anakuna kichwa.

Kuna mahusiano gani kwenye matukio haya mawili? - Kupotea kwa maiti ya mwanamke na ajali mbaya ya mlinzi?

Anataka kujua vema, mwanamke huyu ambaye mwili wake umepotea ni nani.
View attachment 2958963

Anapewa taarifa jina lake ni Mayka, mwanamke wa makamo, mfanyabiashara tajiri ambaye kifo chake kilisababishwa na mshtuko wa moyo.

Mwanamke huyu aliolewa na kijana mdogo kiumri jina lake Alex Ulloa, bwana mmoja anayefundisha huko chuoni, na mwili wake hapa mochwari ulikuwa unangojea kufanyiwa uchunguzi wa kisayansi kubaini ukweli juu ya kifo chake (Autopsy).

Kupata maelezo hayo, inspekta akawa amempata mtuhumiwa wake kwanza kichwani, si mwingine bali Alex Ulloa.
View attachment 2958964

Bwana huyo alipewa taarifa ya kupotea kwa mwili wa mkewe, akafika hospitalini upesi akiwa na bumbuwazi. Ni yeye ndo' aliuleta mwili huu hapa, tena baada ya kuhakikisha kwamba Mayka kafariki, sasa kimetokea nini?

Alex anatoa maelezo na inspekta anamshuku huenda bwana huyu alimuua mkewe kwa sumu kisha akautorosha mwili wake kuepusha uchunguzi.

Lakini huu ndo' ukweli?

HAPANA.

Ni kweli enzi za uhai wake, Mayka alikuwa anampenda sana Alex kiasi cha kufunga naye ndoa pasipo kujali umri wake mkubwa lakini kiuhalisia, kwa Alex hali ilikua tofauti.
View attachment 2958965

Yeye alimpenda huyu 'mshangazi' kwasababu ya pesa tu, na si vinginevyo.

Siku moja Alex akiwa kazini, anakutana na mwanamke anayetokea kumpenda sana, mwanamke kijana kama yeye, aitwaye Carla.
View attachment 2958966
Wanatengeneza mahusiano mazito kiasi kwamba Alex anaanza kupwaya kwa 'mshangazi' wake. Si unajua tena ya mshika mawili?

Na hivi michepuko walivyo na sifa sasa, anazikamua zote, Alex akifika kwa mshangazi hana hata tone. Dhoofu bin taaban!

Mayka akaanza kuhisi kuna mtu anampokonya tonge lake.

Upande wa pili, mchepuko nao ukaanza kutingisha kiberiti - hautaki tena kushea, anaitaka hii tamu iwe yake peke yake.

Sasa Alex anakuwa njia panda.

Bado pesa za mshangazi anazitaka, na raha za mchepuko ndo' usiseme.

Ili apate vyote, anaamua kummaliza 'le mshangaz' kwa kumwekea sumu ya kumuua taratibu ili afe abakiwe na mali na huku pia aendelee na penzi la Carla.

Anafanikiwa vema.

Mayka anakunywa wine yenye sumu na kufariki dunia baada ya siku kadhaa kama vile ilivyopangwa.

Alex anampa taarifa Carla kwamba zoezi limekamilika. Mwili wa Mayka upo mochwari, hauna pumzi tena, na sasa wapo free kula mema ya nchi.
View attachment 2958968

Kwahiyo ni kweli isiyo na shaka, Alex kamuua Mayka. Lakini si kweli kwamba Alex amehusika na kuuchukua mwili wa Mayka mochwari!

Sasa mwili uko wapi?

Mhusika ni nani?

Mara kidogo, mlinzi anapata unafuu wa angalau kuweza kuongea.

Swali la kwanza, ni aliona nini siku ile mpaka akakimbia?

Katazame 'El Cuerpo' (The Body).
View attachment 2958970
Nitakuja
 
Yts inabidi kuwa na Bittorrent halafu kule full kubwakubwa tu japo ni HD ila unakuta movie 1. 9GB
Nitaangalia
Upo nyuma sana kaka. Chukua link huko kisha paste kwenye LJ video downloader. Chagua resolution unayotaka, download.
 
Back
Top Bottom