Binafsi huwa sivutiwi kabisa na muvi au tamuthilia za Bongo.
Hawa jamaa wanapata 'airtime ' kwasababu wabongo tunahuluka ya kufatilia na kushabikia vitu vya kijinga.
Ukiangalia muvi zao hawapo 'smart ' kwenye kila jambo:-
π΄ Poor location; location inaathari kubwa sana kwenye ulimwengu wa filamu hasa Afrika.
Uchaguzi mbaya wa mazingira ya kufanyia filamu mfano wanaigizia uswahilini, mitaa michafu, makazi ya hovyo na yasiyokuwa na mpangilio wa kueleweka.
π΄ Bad acting; wabongo wao wanadhani kuigiza ni kukaa kwenye kochi na kuongea au kufoka.
Kitu kinachopelekea filamu za wazungu wa Uraya magharibi au Marekani zionekane nzuri na zenye mvuto ni kwa sababu ya 'good acting and prot twisting '
π΄ Poor production; Ukifatilia filamu au tamuthilia nyingi za wabongo hawajui ni wapi audience asikie music sound na niwapi hapaswi.
Filamu au tamuthilia nzima imejaa music sounds za kila aina ,nyimbo za majonzi, mapenzi mara vinanda hujakaa sawa unasikia jina la tamuthilia likitajwa katikati wakati lilipaswa lionyeshwe mwanzo wa tamuthilia.
π΄ Poor introduction &bad ending; Ukiangalia tamuthilia za wazungu namuna zinavyoanza ukaangalia na zawabongo utagunduwa kabisa wabongo hawajuwi wanachokifanya kwenye ulimwengu wa filamu.
π΄ Poor script writing; Kwenye uwandishi wa script kuna swala la 'Psychology ' kulingana na mazingira husika, anapositahili kusimama mwalimu anatakiwa kuwa mwalimu kweli kwa sababu kila sehemu inalugha zake za kisaikolojia.
π΄ Poor story telling; Chukulia tamuthilia kama KOMBOLELA ni tamuthilia ambayo inawalenga watu wachache kutoka kwenye jamii fulani.
Hii maana yake ni kuwa wakenya hawapaswi kuitazama.
ni hitimishe kwa kusema ULIMWENGU WA FILAMU HAUWAITAJI WABONGO ,WATAFUTE KAZI ZA KUFANYA.