Johnny Sins
JF-Expert Member
- Nov 4, 2019
- 2,537
- 3,873
Mkongwe kwenye kazi za kimafia na muuaji wa kukodiwa asie na mipaka john wick,anastaafu hiyo kazi baada ya kuoa na kutulia na mkewe.
Baada ya mkewe kuugua ghafla na kufa, John anabaki kwenye huzuni kubwa na maisha yakaendelea akiwa na zawadi ya mbwa alioachiwa na mkewe kama kumbukumbu.
Mtoto mmoja muhuni wa tajiri anamuona John Wick sheli na kumwambia amuuzie gari lake, John anakataa.
Yule kijana akafanya kosa la kumfatilia John mpaka nyumbani kwake na wenzie na kumpiga kipigo cha mbwa mwizi wakitafuta funguo za gari, wakafanya kosa lingine kubwa zaidi, wakamuua mbwa wake.
Walipopeleka gari gereji likabadilishwe. Mwenye gereji akawafukuza sababu gari analijua ni la nani. Yule kijana alipoenda kwa baba yake ambaye ni tajiri na ni muuaji pia, akamwelezea, baba mtu akashtuka; akamuuliza mtoto wake"umechukua gari la nani? Mtoto akajibu "aah baba lile si gari tu na yule ni mnyonge"
Baba akafoka akasema kwa sauti, lile sio gari, lile ni gari la John Wick.
Mtoto akauliza "John Wick ni nani"?
Baba akamnasa kwanza kofi mwanae halafu akaanza kumwambia kuhusu huyo John Wick, huku akimwambia mwanangu umeyakanyaga, kaandae jeshi mpaka kutoka Australia, umeamsha jini.
Alipoambiwa kuwa na mbwa wake tumemuua; mzee sigara ilimtoka mdomoni, anamjua vizuri huyo mtu.
Muda huo John Wick baada ya kuamka alipopigwa, akaamka akiwa yule John Wick waliemsahau. Mnyama, binadamu mwenye roho mbaya kuliko roho mbaya yenyewe.
Rafiki yake John Wick askari akamwambia hawa vijana ntawakamata, John akamuuliza "umenisahau" yule askari akatetemeka, aksema kazi imeanza, maaskari waanze kuokota maiti, sababu ni mbwa tu.
Kweli jiji lilizima. Mji ulichafuka. Dunia ilijua..
ITS JOHN WICK MOVIE SERIES