Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 37,630
- 47,434
Tunaambiwa kwamba filamu ya Royal Tour yenye kupromote Utalii imegharimu Shilingi za Kitanzania Bilioni tisa. (9).
Leo tunaambiwa Rais ana safari ya kikazi yeye na delegation yake marekani na moja wapo ya mambo atayoyafanya ni kuzindua filamu ya Roya Tour.
Kwakua hizo kazi nyingine atazofanya hatujaambiwa ni zipi hivyo main task inakuwa ni Kuzindua filamu yake.
Ukiachana na matumizi ya Bilioni Tisa kwenye maandalizi ya filamu bado tunatumia tena mapesa mengine kwenye Uzinduzi na badala ya kuufanya hapa nyumbani tunaufanyia Marekani.
Matumizi ya mapesa haya yanafanyika kipindi tukiwa kwenye wave ya Corona maana tumeambiwa ipo na Vita Vya Ukraine.
Ukiachana na uwepo wa korona na vita ya Ukraine , Uchumi wetu umekumbwa na pigo la kupanda kwa bei za bidhaa muhimu jambo linaloongeza ukali wa Maisha kwa wananchi wa kawaida.
Inaleta ukakasi wa matumizi ya aina hii ya mapesa wakati Taifa likipitia kipindi kigumu namna hii.
Sijui viongozi wetu wanafikiria nini ila haipendezi kuzindua Filamu huko ughaibuni kwa mapesa mengi wakati kuna mtanzania hapa hata mlo wake tu unakua wa kuvizia na wakati juzi tu hapa Waziri Ummy anatuletea takwimu kwamba bado kuna idadi ya watanzania wanaojisaidia maporini(hawana vyoo)
Ningeiomba tu Serikali ijaribu kubana matumizi hasa kipindi hiki badala ya kuendelea kutumia fedha ambazo hatuna kwa mambo ambayo yanaonekana kabisa yasingefaa kufanyika kwa kipindi hiki.
Vile vile timing ya uzinduzi nayo sio nzuri maana jumuia za kimataifa zinahangaika na vita vya Urusi na Ukraine hivyo mwamko wa filamu hiyo utakua mdogo.
Wangesubiri mambo yatulie kidogo kama kweli tunataka kuipromote hiyo video.
Asanteni.
On top of that,
Uzinduzi unafanyika Marekani kuvutia watalii wakati Taifa la Marekani limekataza Raia wake kuja Tanzania kutokana na uwepo wa Korona.
tz.usembassy.gov