Filamu ya Royal Tour Ingezinduliwa Tanzania Badala ya Marekani kuepuka gharama

Filamu ya Royal Tour Ingezinduliwa Tanzania Badala ya Marekani kuepuka gharama

Tunaambiwa kwamba filamu ya Royal Tour yenye kupromote Utalii imegharimu Shilingi za Kitanzania Bilioni tisa. (9).

Leo tunaambiwa Rais ana safari ya kikazi yeye na delegation yake marekani na moja wapo ya mambo atayoyafanya ni kuzindua filamu ya Roya Tour.

Kwakua hizo kazi nyingine atazofanya hatujaambiwa ni zipi hivyo main task inakuwa ni Kuzindua filamu yake.

Ukiachana na matumizi ya Bilioni Tisa kwenye maandalizi ya filamu bado tunatumia tena mapesa mengine kwenye Uzinduzi na badala ya kuufanya hapa nyumbani tunaufanyia Marekani.

Matumizi ya mapesa haya yanafanyika kipindi tukiwa kwenye wave ya Corona maana tumeambiwa ipo na Vita Vya Ukraine.

Ukiachana na uwepo wa korona na vita ya Ukraine , Uchumi wetu umekumbwa na pigo la kupanda kwa bei za bidhaa muhimu jambo linaloongeza ukali wa Maisha kwa wananchi wa kawaida.

Inaleta ukakasi wa matumizi ya aina hii ya mapesa wakati Taifa likipitia kipindi kigumu namna hii.

Sijui viongozi wetu wanafikiria nini ila haipendezi kuzindua Filamu huko ughaibuni kwa mapesa mengi wakati kuna mtanzania hapa hata mlo wake tu unakua wa kuvizia na wakati juzi tu hapa Waziri Ummy anatuletea takwimu kwamba bado kuna idadi ya watanzania wanaojisaidia maporini(hawana vyoo)

Ningeiomba tu Serikali ijaribu kubana matumizi hasa kipindi hiki badala ya kuendelea kutumia fedha ambazo hatuna kwa mambo ambayo yanaonekana kabisa yasingefaa kufanyika kwa kipindi hiki.

Vile vile timing ya uzinduzi nayo sio nzuri maana jumuia za kimataifa zinahangaika na vita vya Urusi na Ukraine hivyo mwamko wa filamu hiyo utakua mdogo.

Wangesubiri mambo yatulie kidogo kama kweli tunataka kuipromote hiyo video.

Asanteni.

Nadhani awajatengeneza movie iyo kwa ya Tanzania, ni kwa ajili ya dunia kutambua kwetu tuna nini!

Binafsi, naona wako sawa kuizindua marekani...
 
Timing ni mbaya.

Kwasasa Vita vya ukaraine ndio ina make headlines.

Hiyo filamu haitapata attention inayokusudiwa.

Angesubiri basi hata vita iishe. Uchumi uimarike aiachie haraka ya nini??
Vita ya Ukraine haina headline ya maana Sasa hivi. Maisha lazima yaendelee. Waje tupate hela za kigeni.
 
Nadhani awajatengeneza movie iyo kwa ya Tanzania, ni kwa ajili ya dunia kutambua kwetu tuna nini!

Binafsi, naona wako sawa kuizindua marekani...
Kama ni kwa ajili ya Dunia basi sio lazima iwe marekani hata hapa pia ingefaa tu.
 
Au huna habari kuna mamia ya watalii toka Ukraine walikwama hapa.

Hapa nazungumzia attention ya dunia iko wapi kwa sasa.

Watu wanapambana na vita na madhara yake na korona pia.

Wrong timing again.
Marekani watu hawafuatilii sana vita, wako busy sana kufanya kazi. Mwitikio ni mkubwa sana. Kule marekani kila mahali Bahamas wameweka video zao na wanaongoza kwa utalii maeneo ya Caribbean yote. Acha na sisi tuchangamkie fursa. Video iende viral.
 
Sidhani kama tutafikia malengo wakati huu korona ikiwa imeshika kasi.
 
Walengwa ni wageni toka Ulaya na Marekani,sasa ikizinduliwa Tz hao walengwa wataijuaje?
 
Yani filamu ya bilioni 7 ukazindue mlimani city?

Walengwa ni watalii wa nje
 
Walengwa ni wageni toka Ulaya na Marekani,sasa ikizinduliwa Tz hao walengwa wataijuaje?
Basi ipo haja ya kwenda Ulaya pia ili malengo yatimie maana watalii hawapo marekani pekee.
 
Huu ndio muda mzuri maana watu wanataka kuondoka kule, restrictions za Corona hawazitaki.
Huu sio muda mzuri maana kuna travel restrictions.

Hata hivyo bado Marekani sio suitable choice maana Marekani imekataza Raia wake kuja kutembelea tanzania kwakua kuna janga la korona.

Sasa unakwenda kuzindua filamu kwa watu ambao hawataki kuja kwako??

Angalia website ya Ubalozi wa marekani hapa.

Tanzania ipo level 4. Kwamba mtu hatakiwi kuja hapa.

Screenshot_20220413-232427.png
 
Badili hata ID maana kwa ID hi, kila utakachoongea utaonekana Ni njaa inakusumbua.

Bora hata huyo Samia anapambania kutafuta watalii, Kibwengo magufuli aliyekuwa anatumia mabilioni ya walipa Kodi kufurahisha nafsi yake tu.

Budget ya NEC kwa Jimbo moja la uchaguzi Ni Milioni 300.

Tulifanya CHAGUZI karibu 30 za kijuha juha tu eti watu wanting mkono Juhudi.

Leo, kina Mnyeti, Sabaya, Bashite, Kalemani na Genge lote la Magu Ni MATAJIRI wa KUTISHA kabisa.
Eti kibwengo 😂
 
Huu sio muda mzuri maana kuna travel restrictions.

Hata hivyo bado Marekani sio suitable choice maana Marekani imekataza Raia wake kuja kutembelea tanzania kwakua kuna janga la korona.

Sasa unakwenda kuzindua filamu kwa watu ambao hawataki kuja kwako??

Angalia website ya Ubalozi wa marekani hapa.

Tanzania ipo level 4. Kwamba mtu hatakiwi kuja hapa.

View attachment 2186612
Hata hivyo Putin anachukua Nobel prize mwaka huu kwenye medicine maana ameimaliza Corona duniani kwa kuivamia Ukraine.

Usiogope, watalii wanakuja kutoka marekani. Kule ndio kuna watu wenye hela za kutumia for fun.
 
Wamarekani hawawezi kuja kwakua wanaisikiliza serikali yao iliyowaambia kuwa hapa Tanzania kuna Korona, Ugaidi na pia hatuzingatii haki za Mashoga.

Au huelewi kingereza.
 
Back
Top Bottom